Klabu ya Barcelona imethibitisha rasmi kuwa winga wake raia wa Brazil, Raphinha, ameongeza mkataba mpya utakaomuweka ndani ya kikosi hicho hadi Juni 2030.
Hatua hiyo inaonyesha dhamira ya Barcelona kuendelea kumtegemea nyota huyo kwa miaka mingine minne, kufuatia mchango wake mkubwa ndani ya timu hiyo.
Raphinha anasaini mkataba huo akiwa katika kiwango bora msimu huu, akiwa amecheza michezo 13 na kufunga mabao 19.
Kwa makubaliano hayo, Barcelona imehakikisha inaendelea kuwa na huduma ya mmoja wa wachezaji wake muhimu katika miaka ijayo. Raphinha bado yupo Barcelona!
ADVERTISE HERE