Young Africans (Yanga) imefikia makubaliano ya maslahi binafsi na kocha raia wa Afrika Kusini, Fadlu Davids, kwa ajili ya kumkabidhi jukumu la kuinoa timu hiyo.
Kwa sasa, pande hizo zinaendelea na taratibu nyingine za kukamilisha dili hilo kabla ya kutangazwa rasmi kwa Davids kama kocha Mkuu wa Yanga.
Davids anaifahamu vyema soka la Tanzania, kwani aliwahi kuwa kocha wa Simba SC kabla ya kuondoka nchini na kujiunga na klabu ya Raja Casablanca ya Morocco.
Iwapo makubaliano hayo yatakamilika, Davids atarejea Tanzania akiwa na jukumu la kuiongoza Yanga, safari hii akiwa upande wa watani wa jadi wa klabu aliyowahi kuifundisha.
ADVERTISE HERE