Michezo ya saa 20:45 katika UEFA Champions League imemalizika kwa matokeo yenye msisimko, huku Liverpool ikipoteza kwa mabao 3-2 dhidi ya Fenerbahce nchini Uturuki, wakati Real Madrid ikipata ushindi wa mabao 3-2 ugenini dhidi ya AEK Athens.
Katika mchezo uliopigwa Uturuki, Fenerbahce iliandika ushindi huo kupitia mabao ya Mason Greenwood dakika ya 29, Archie Brown dakika ya 73 na Muriqi dakika ya 79. Liverpool ilipata mabao yake kupitia Nyoni dakika ya 25 na Alexander Isak dakika ya 69, lakini haikuweza kuzuia wenyeji kupata pointi tatu.
Kwa upande mwingine, Real Madrid ililazimika kupambana hadi dakika za mwisho kupata ushindi dhidi ya AEK Athens. Wenyeji walitangulia kupata bao kupitia Koita dakika ya 12, kabla ya Jude Bellingham kusawazisha dakika ya 32.
Pillios aliirudisha AEK Athens mbele dakika ya 75, lakini Kylian Mbappe akasawazisha tena dakika ya 78. Federico Valverde akawa shujaa wa Real Madrid kwa kufunga bao la ushindi dakika ya 90+2 na kuifanya timu hiyo kuondoka na ushindi wa mabao 3-2..jpg)
Matokeo kamili
Fenerbahce 3-2 Liverpool
AEK Athens 2-3 Real Madrid