Michezo ya UEFA Champions League imeendelea kwa matokeo mbalimbali, huku Manchester United ikiandika simulizi la kusisimua baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya AS Roma kufuatia mchezo uliojaa mabadiliko ya matokeo.
Roma ilianza kwa kasi na kupata mabao mawili dakika ya 11 na 18, hali iliyowafanya Manchester United kwenda mapumziko ikiwa nyuma kwa mabao 2-0. Kipindi cha pili United ilipata penalti dakika ya 56, lakini Bruno Fernandes alikosa nafasi ya kwanza kabla ya kufunga penalti iliyorudiwa dakika ya 58.
Mchezo uliendelea kuwa mkali, huku Mbeumo akikaribia kusawazisha lakini shuti lake likigonga nguzo zote mbili. Hata hivyo, Matheus Cunha aliibuka shujaa kwa kufunga mabao dakika ya 82 na 86 na kuipa United ushindi wa 3-2, kabla ya kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 90 na moja.
Katika michezo mingine, Paris Saint-Germain iliibuka na ushindi mkubwa wa mabao 6-0 dhidi ya Villarreal, huku Barcelona ikiichapa Aston Villa mabao 3-0. Raphinha alifunga mabao mawili dakika ya 52 na 64, huku Lamine Yamal akifunga dakika ya 7.
Bayern Munich nayo iliichapa Atletico Madrid mabao 2-0 kupitia Karl dakika ya 54 na Laimer dakika ya 74. Inter Milan ilipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Feyenoord, huku Bisseck, Esposito na Zielinski wakifunga dakika za 8, 34 na 54 mtawalia.
Galatasaray iliifunga Stuttgart mabao 2-0 kupitia Aleksey Batrakov dakika ya 12 na 15, wakati Sporting CP ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Shakhtar Donetsk kupitia Issa Doumbia dakika ya 59.
LASK ilipata ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Slovan Bratislava, huku Bodo/Glimt na Lille zikitoshana nguvu kwa sare ya bila kufungana.

Matokeo yote
Saa 2:45 usiku
Galatasaray 2-0 Stuttgart
Shakhtar Donetsk 0-1 Sporting CP
Saa 5:00 usiku
Atletico Madrid 0-2 Bayern Munich
Barcelona 3-0 Aston Villa
Bodo/Glimt 0-0 Lille
Feyenoord 0-3 Inter Milan
LASK 4-0 Slovan Bratislava
Villarreal 0-6 PSG
Manchester United 3-2 AS Roma