Klabu ya West Ham United imetangaza kumfuta kazi kocha wake Nuno Espírito Santo kuanzia mara moja, kufuatia mwenendo usioridhisha wa matokeo ya timu hiyo.
Uamuzi huo umefikiwa wakati West Ham ikiwa nafasi ya nane katika msimamo wa Championship, hali iliyoifanya klabu hiyo kuchukua hatua ya kuachana na kocha huyo.
Kupitia taarifa yake, West Ham imethibitisha rasmi kuvunjwa kwa mkataba wa Nuno, huku ikitarajiwa kuanza mchakato wa kutafuta kocha mpya atakayeiongoza timu hiyo katika kipindi kilichosalia cha msimu.
ADVERTISE HERE