Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo kwa michezo miwili inayotarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wa soka nchini, huku Young Africans ikiwa miongoni mwa timu zitakazokuwa dimbani kusaka pointi tatu.
Mchezo wa kwanza utakuwa kati ya Polisi Tanzania dhidi ya Geita Gold, utakaopigwa saa 10:00 jioni katika Uwanja wa Ushirika, Kilimanjaro.
Baadaye, saa 1:00 usiku, Young Africans itashuka dimbani katika Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam, kuvaana na Kagera Sugar katika mchezo mwingine unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Ni michezo miwili, lakini kila timu inaingia uwanjani ikiwa na dhamira ya kupata matokeo mazuri.
ADVERTISE HERE