Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta, anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Le Havre kitakachokuwa na kibarua kigumu dhidi ya Paris Saint-Germain (PSG), katika mchezo wa raundi ya tisa ya Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1), utakaopigwa leo, Ijumaa, Oktoba 30, 2026. Pambano hilo litafanyika katika Uwanja wa Stade Océane, nyumbani kwa Le Havre, likiwa na umuhimu mkubwa kwa timu zote mbili kutokana na malengo tofauti wanayoyafukuzia msimu huu.
Le Havre wanaingia katika mchezo huo wakiwa katika wakati mgumu, kufuatia kuwa katika nafasi ya mwisho 18 katika ligi kuu ya nchini ufaransa ikiwa na alama mbili pekee baada ya kucheza michezo 8.
Kwa upande wa Paris Saint-Germain wanaingia katika mchezo huu wakiwa na dhamira ya kuendeleza ubabe wao katika ligi hiyo ambayo hadi hivi sasa wako kileleni mwa msimamo wakiwa na alama 17 baada ya kucheza michezo 8 ikikusanya alama 17.
Kwa Le Havre, changamoto kubwa itakuwa namna ya kuzuia mashambulizi ya PSG huku wakitafuta mianya ya kuadhibu wapinzani wao. Timu hiyo pia inakabiliwa na changamoto ya majeruhi, akiwemo kipa Lionel Mpasi-Nzau. huku upande wa PSG wanatajwa kuwa na mapungufu ya kikosi kutokana na kutokuwepo kwa Ousmane Dembélé na Nuno Mendes, jambo linaloweza kuathiri mipango ya kocha wao katika mchezo huo.