Viongozi wa Barcelona wanadaiwa kutoridhishwa na uamuzi wa kocha wa timu ya taifa ya Brazil, Carlo Ancelotti, kumjumuisha Raphinha kwenye kikosi kitakachocheza mchezo wa kirafiki nchini Singapore mwezi Novemba.
Winga huyo amerejea hivi karibuni kwenye utimamu wa mwili baada ya kupona jeraha alilolipata wakati wa mapumziko ya awali ya mechi za kimataifa.
Hali hiyo imezua wasiwasi ndani ya Barcelona, ambayo inahofia kumruhusu Raphinha kusafiri tena kwa majukumu ya timu ya taifa muda mfupi baada ya kurejea uwanjani.
Klabu hiyo inatajwa kuwa na hofu ya uwezekano wa mchezaji huyo kupata jeraha jingine, jambo ambalo linaweza kuathiri mipango yao katika michezo ijayo.
Kwa sasa, suala la ushiriki wake kwenye majukumu ya kimataifa linaweza kuwa changamoto kwa Barcelona, ambayo inahitaji huduma ya nyota huyo akiwa katika kiwango bora.