Cristiano Ronaldo ameendelea kuikaribia rekodi ya kufikisha mabao 1,000 katika maisha yake ya soka baada ya kufunga hat-trick katika ushindi wa Al-Nassr wa mabao 5-3 dhidi ya Al-Kholood jana.
Ronaldo alifunga mabao matatu, huku nyota mwenzake kutoka Ureno, João Félix, akitoa pasi nne za mabao katika mchezo huo na kuonyesha kiwango bora.
Kwa sasa, Ronaldo amebakiza mabao 15 pekee kufikisha idadi ya mabao 1,000, rekodi ambayo imekuwa moja ya malengo makubwa katika hatua hii ya maisha yake ya soka.
ADVERTISE HERE