Yanga mbioni kumrejesha Sead Ramovic

Joel JJ By Joel JJ
β€’
5h ago
Yanga mbioni kumrejesha Sead Ramovic

Mashabiki wa Yanga huenda wakapata kile walichokuwa wakikitamani baada ya taarifa kueleza kuwa uongozi wa klabu hiyo umefikia makubaliano ya kumrejesha kocha wa zamani, Sead Ramovic, kurithi mikoba ya Manqoba Mngqithi aliyefutwa kazi wiki iliyopita.

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga zinaeleza kuwa makubaliano yamefikiwa na kinachosubiriwa ni hatua za mwisho kabla ya kocha huyo kutangazwa rasmi.

Inaelezwa kuwa Ramovic anaweza kuwasili nchini leo kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kusaini mkataba na kuanza majukumu yake katika awamu ya pili ya kuitumikia klabu hiyo ya Jangwani.

Sead Ramovic si jina geni kwa mashabiki wa Yanga. Kocha huyo aliwahi kuitumikia klabu hiyo katika msimu wa 2024/25, akivutia sehemu ya mashabiki kupitia falsafa yake ya soka na namna alivyotaka kikosi chake kucheza.

Hata hivyo, safari yake ya kwanza Yanga haikudumu kwa muda mrefu baada ya kuondoka na kujiunga na CR Belouizdad ya Algeria, ambayo ilivunja mkataba wake na Wananchi.

Uwezekano wa kurejea kwake sasa umeibua matumaini miongoni mwa mashabiki wanaoamini kuwa kocha huyo anaweza kuendeleza kazi aliyoianza kabla ya kuondoka.

Mashabiki walivyotaka Ramovic na Behlulovic warejee

Baada ya uongozi wa Yanga kuachana na Manqoba Mngqithi, mashabiki wengi walielekeza maoni yao kwenye mitandao ya kijamii wakimtaka Ramovic na kocha wa viungo Adnan Behlulovic.

Baadhi yao walimwomba Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said, kuangalia uwezekano wa kuwarejesha makocha hao ili kuimarisha benchi la ufundi la klabu hiyo.

Iwapo atathibitishwa rasmi, Ramovic atakabiliwa na jukumu la kuijenga upya timu na kuhakikisha kikosi kinakuwa tayari kwa changamoto zinazokikabili katika mashindano ya ndani na kimataifa.

Yanga ina malengo makubwa ya kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League), hivyo kupata kocha mapema kutakuwa muhimu katika maandalizi ya kikosi, mbinu za mchezo na kujenga muunganiko kati ya wachezaji.

Falsafa yake inayotajwa na mashabiki kwa kauli ya “Gusa, achia, twende kwao,” ni miongoni mwa mambo yanayowafanya baadhi yao kutamani kurejea kwake.

ADVERTISE HERE

More Stories

Simba yataja nafasi za kugombea uongozi uchaguzi mkuu Januari 2027
Simba yataja nafasi za kugombea uongozi uchaguzi mkuu Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Mangungu awatupia lawama washauri wa Dewji kufuatia kukwama kwa uwekezaji Simba
Mangungu awatupia lawama washauri wa Dewji kufuatia kukwama kwa uwekezaji Simba
2h ago
READ MORE β†’
Jay-Z aingilia kati baada ya polisi kuitwa kwenye mechi ya mtoto!
Jay-Z aingilia kati baada ya polisi kuitwa kwenye mechi ya mtoto!
3h ago
READ MORE β†’
Oktoba 31 mwisho wa usajili wa wachezaji wa ziada Caf
Oktoba 31 mwisho wa usajili wa wachezaji wa ziada Caf
3h ago
READ MORE β†’
Simba sc kumtangaza CEO hivi karibuni Mangungu athibitisha
Simba sc kumtangaza CEO hivi karibuni Mangungu athibitisha
4h ago
READ MORE β†’
Mangungu: mchakato wa uchaguzi Simba ni batili na haramu
Mangungu: mchakato wa uchaguzi Simba ni batili na haramu
4h ago
READ MORE β†’
Liverpool kukutana na Bournemouth, Man City kuivaa Bradford robo fainali Carabao Cup
Liverpool kukutana na Bournemouth, Man City kuivaa Bradford robo fainali Carabao Cup
5h ago
READ MORE β†’
Ligi Kuu NBC, mechi nne kupigwa leo
Ligi Kuu NBC, mechi nne kupigwa leo
6h ago
READ MORE β†’
Azam Fc inagawa dozi tu Chamazi, yaichapa Mbeya City 4-0
Azam Fc inagawa dozi tu Chamazi, yaichapa Mbeya City 4-0
9h ago
READ MORE β†’
Mchakato wa uchaguzi Simba hadharani
Mchakato wa uchaguzi Simba hadharani
10h ago
READ MORE β†’