Klabu ya Simba SC ya Tanzania imeendelea kuimarisha hadhi yake katika soka la Afrika baada ya kuingizwa kwenye orodha ya klabu zilizoshiriki mara nyingi zaidi hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League).
Kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Simba SC inashika nafasi ya 12 ikiwa imefuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo mara saba (7).
Idadi hiyo inaiweka sambamba na klabu ya Enyimba FC ya Nigeria. Orodha hiyo inaongozwa na EspΓ©rance de Tunis ya Tunisia iliyoshiriki hatua ya makundi mara 24, ikifuatiwa na Al Ahly ya Misri yenye ushiriki mara 23.
Al Hilal ya Sudan inashika nafasi ya tatu ikiwa imeshiriki mara 15. Rekodi hiyo inaonesha mwendelezo wa Simba SC katika mashindano makubwa zaidi ya klabu barani Afrika na mafanikio ambayo klabu hiyo imeendelea kuyapata katika jukwaa la kimataifa.
Wekundu wa Msimbazi wanaendelea kuwa miongoni mwa wawakilishi muhimu wa Tanzania katika soka la Afrika, huku ushiriki wao wa mara kwa mara katika CAF Champions League ukiendelea kujenga hadhi ya klabu hiyo kwenye michuano ya kimataifa.