Klabu ya Yanga SC inatajwa kumuwania kocha wa zamani wa Pyramids FC ya Misri, Krunoslav Jurcic, kufuatia kuachana na kocha Manqoba Mngqithi.
Kocha huyo raia wa Croatia anaripotiwa kuwa miongoni mwa majina yanayozingatiwa na viongozi wa klabu hiyo katika mipango ya kuimarisha benchi la ufundi na kuongeza ushindani katika mashindano ya kimataifa.
Kwa mujibu wa taarifa, Yanga imeanza kutafuta kocha atakayechukua nafasi hiyo huku jina la Jurcic likitajwa kuingia katika mipango ya klabu hiyo.
Jurcic ni kocha mwenye uzoefu wa soka la ushindani, hasa katika mazingira ya mashindano ya vilabu barani Afrika. Uzoefu wake akiwa na Pyramids FC umechangia jina lake kuhusishwa na klabu zinazotaka kujenga timu yenye ushindani katika ngazi ya kimataifa.
Jurcic alijenga jina lake kupitia kazi yake na Pyramids FC, klabu ya Misri iliyokuwa ikisaka mafanikio makubwa katika mashindano ya ndani na ya kimataifa.
Katika kipindi chake na timu hiyo, aliiwezesha Pyramids kuimarisha nafasi yake katika soka la Afrika, huku akiingoza timu hiyo kushinda mataji matano miongoni likiwa taji la ligi ya mabingwa (CAFCL).
Pamoja na kocha huyo, Yanga pia inatajwa kufanya mazungumzo na kocha wa zamani wa klabu za Simba na Raja CA, Fadlu Davids.
Kwa sasa benchi la ufundi la Yanga linaongozwa na Simo Dladla ambaye alikuwa sehemu ya benchi la ufundi la Manqoba akiwa kocha msaidizi.