Klabu ya Young Africans SC imeamua kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Manqoba Mngqithi, pamoja na kusitisha mkataba wa kocha wa viungo, Chyna Mokaila, kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo.
Uamuzi huo unakuja wakati Yanga ikikabiliwa na changamoto ya matokeo yasiyoridhisha katika michezo yake ya hivi karibuni, hali iliyochangia mabadiliko hayo katika benchi la ufundi.
Kupitia taarifa yake, uongozi wa Yanga umewashukuru makocha hao kwa mchango wao ndani ya klabu na kuwatakia kila la kheri katika majukumu yao mapya.
Aidha, Yanga imesema tayari imeanza mchakato wa haraka wa kumpata kocha mkuu mpya, huku ikitarajia kukamilisha zoezi hilo hivi karibuni. Sasa macho ya mashabiki wa Wananchi yataelekezwa kwa uongozi kuona nani atapewa jukumu la kuiongoza timu hiyo katika kipindi kijacho.