Villa, PSG, Madrid mambo mazuri katika usiku wa UEFA.

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
β€’
2h ago
Villa, PSG, Madrid mambo mazuri katika usiku wa UEFA.

Michezo ya UEFA Champions League iliyochezwa leo imeshuhudia matokeo ya kuvutia, ushindi mkubwa na mabao mengi katika viwanja mbalimbali. Aston Villa imeonyesha ubabe kwa kuichapa Fenerbahce mabao 6-0, huku Paris Saint-Germain ikiibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Manchester City katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Katika mchezo wa saa 19:45, Feyenoord imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Como. Assane Diao aliifungia Como bao la kwanza dakika ya 18, lakini Zechiel aliisawazishia Feyenoord dakika ya 20. Hadj Moussa aliipa Feyenoord bao la pili dakika ya 52, kabla ya bao la kujifunga la Roberto Sanchez dakika ya 81 kuongeza bao la tatu. Douvikas aliifungia Como bao la pili dakika ya 90 na 3, lakini halikutosha kuzuia ushindi wa Feyenoord.Katika mchezo mwingine wa saa 19:45, LASK imepoteza kwa mabao 5-3 dhidi ya Liverpool katika pambano lililokuwa na mabao mengi. Ronald Araujo aliifungia Liverpool dakika ya 22, kabla ya Bradley Barcola kufunga mabao matatu dakika ya 24, 37 na 66. Robert Ljubicic aliifungia LASK dakika ya 63, huku Florian Flecker akiongeza mabao mawili dakika ya 74 na 77. Lewis Koumas aliifungia Liverpool bao jingine dakika ya 72, na kuifanya timu hiyo ipate ushindi wa mabao 5-3.Michezo ya saa 22:00 ilianza kwa Aston Villa kuonyesha ubora wake kwa kuichapa Fenerbahce mabao 6-0. Manzambi alianza kufunga dakika ya 12, kabla ya Nicolas Jackson kuongeza mabao mawili dakika ya 31 na 39. Ross Barkley aliendelea kuimarisha ushindi huo kwa kufunga dakika ya 68 na 72, huku Tammy Abraham akihitimisha karamu ya mabao dakika ya 90.Bodo Glimt imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Borussia Dortmund. Fredrik Sjovold ndiye aliyekuwa shujaa wa mchezo huo baada ya kufunga bao pekee dakika ya 52, lililoiwezesha timu yake kupata ushindi muhimu.Paris Saint-Germain imeibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Manchester City katika mchezo mwingine uliovuta hisia za mashabiki. Desire Doue aliifungia PSG dakika ya 13, kabla ya Dembele kuongeza bao la pili dakika ya 15. Vitinha aliifanya PSG kuwa mbele kwa mabao matatu dakika ya 32. Manchester City ilijibu kupitia Erling Haaland dakika ya 53, lakini Akliouche aliiongezea PSG bao la nne dakika ya 63. Haaland alifunga bao lake la pili dakika ya 75, lakini halikutosha kuizuia PSG kuondoka na ushindi.Real Betis imepata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya FC Porto katika mchezo mwingine wenye ushindani. Ezzalzouli aliifungia Betis dakika ya 47, kabla ya Gabriel Viega kuisawazishia Porto dakika ya 54. Samuel Aghehowa aliipa Porto bao la pili dakika ya 61, lakini Juan Hernandez aliisawazishia Betis dakika ya 74. Isco alifunga bao la ushindi dakika ya 84 na kuipa Betis ushindi wa mabao 3-2.Real Madrid imeibuka na ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya AS Roma katika mchezo wenye mabao mengi. Marten de Roon aliifungia Roma dakika ya 20, lakini Kylian Mbappe aliisawazishia Real Madrid dakika ya 25. Donyell Malen aliifungia Roma mabao mawili dakika ya 51 na 57. Real Madrid ilijibu kupitia Carlos Espi dakika ya 83 na Endrick dakika ya 85, kabla ya Antonio Rudiger kufunga bao la ushindi dakika ya 90 na kuipa timu yake ushindi wa mabao 4-3.Shakhtar Donetsk imepata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya AEK Athens. Pedrinho aliifungia Shakhtar bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti dakika ya 34, lakini Lovro Majer aliisawazishia AEK Athens dakika ya 28. Vinicius Tobias aliipa Shakhtar bao la pili dakika ya 80, kabla ya Gleiker Mendoza kufunga bao la tatu dakika ya 86 na kuhakikisha timu yake inaondoka na ushindi.Katika mchezo wa mwisho, VfB Stuttgart imeichapa Slovan Bratislava mabao 3-0. Undav alianza kufunga dakika ya 29, kabla ya Cruz kujifunga dakika ya 65 na kuongeza bao la pili kwa Stuttgart. Demirovic alihitimisha ushindi huo dakika ya 90 kwa kufunga bao la tatu.

ADVERTISE HERE

More Stories

UEFA Champions League kuendelea leo kwa mechi tisa za kibabe
UEFA Champions League kuendelea leo kwa mechi tisa za kibabe
13h ago
READ MORE β†’
Baleke atamba, Simba haijapata mshambuliaji wa kumzidi
Baleke atamba, Simba haijapata mshambuliaji wa kumzidi
13h ago
READ MORE β†’
Barcelona na Arsenal zatamba Bayern ikiambulia sare katika usiku wa Uefa.
Barcelona na Arsenal zatamba Bayern ikiambulia sare katika usiku wa Uefa.
14h ago
READ MORE β†’
Zanzibar yafungua milango ya vipaji vya vijana kupitia Real madrid foundation
Zanzibar yafungua milango ya vipaji vya vijana kupitia Real madrid foundation
14h ago
READ MORE β†’
Keffe D ahukumiwa kifungo cha miaka 40 hadi maisha mauaji ya Tupac
Keffe D ahukumiwa kifungo cha miaka 40 hadi maisha mauaji ya Tupac
18h ago
READ MORE β†’
Simba yaichakaza Mashujaa 6-1, Mpanzu atupia mawili.
Simba yaichakaza Mashujaa 6-1, Mpanzu atupia mawili.
1d ago
READ MORE β†’
Highlights : Simba 6-1 Mashujaa Fc
Highlights : Simba 6-1 Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Ally Kamwe awaomba Wanayanga subira, asema maoni yao yatafanyiwa kazi
Ally Kamwe awaomba Wanayanga subira, asema maoni yao yatafanyiwa kazi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yapata pigo, Abuya nje wiki mbili hadi tatu
Yanga yapata pigo, Abuya nje wiki mbili hadi tatu
1d ago
READ MORE β†’
Israel Mwenda karibu kurejea Yanga baada ya Kutatuliwa kwa sakata lake
Israel Mwenda karibu kurejea Yanga baada ya Kutatuliwa kwa sakata lake
1d ago
READ MORE β†’