Baleke atamba, Simba haijapata mshambuliaji wa kumzidi

Joel JJ By Joel JJ
β€’
1h ago
Baleke atamba, Simba haijapata mshambuliaji wa kumzidi

Aliyekuwa mshambuliaji wa Simba SC, Jean Baleke, amezua mjadala katika ulimwengu wa soka nchini baada ya kutamba kuwa, tangu yeye na Moses Phiri walipoondoka klabuni hapo, Wekundu wa Msimbazi bado hawajafanikiwa kupata mshambuliaji wa kati mwenye uwezo mkubwa wa kufumania nyavu kumzidi yeye.

Baleke, ambaye kwa sasa yuko huru baada ya kumalizana na klabu yake ya mwisho, amefunguka hayo huku akisisitiza kuwa viwango vilivyoonyeshwa na safu ya ushambuliaji ya Simba tangu aondoke vimebaki kuwa vya kawaida sana ikilinganishwa na madhara aliyokuwa anayasababisha yeye akiwa ndani ya boksi.

Katika kauli yake iliyozua gumzo kubwa mitandaoni na kwenye vilinge vya soka, mshambuliaji huyo raia wa DR Congo amesema mapengo yaliyoachwa na yeye pamoja na Mzambia Moses Phiri yamekuwa makubwa mno na ndio maana klabu hiyo imekuwa ikihaha kusajili washambuliaji wapya kila msimu bila kupata suluhu ya kudumu.

"Tangu mimi na Phiri tuondoke Simba, sijaona mshambuliaji aliyekuja pale na kuonyesha makali ya kutisha ya ufungaji kutuzidi. Simba bado inatafuta mtu wa aina yetu," alisema Baleke kwa kujiamini.

Kauli ya Baleke inakuja wakati ambao Simba imekuwa ikikosolewa kwa kukosa "muuaji wa kisoka" (clinical finisher) tangu kuondoka kwake mwezi Januari 2024.

Baada ya kuondoka kwake, Simba iliwasajili washambuliaji kama Freddy Michael Kouablan na Pa Omar Jobe ambao walishindwa kufikia matarajio ya mashabiki.

Hata katika misimu ya hivi karibuni, ingawa klabu hiyo imekuwa ikifanya maboresho makubwa kwenye safu yake ya ushambuliaji, bado wachambuzi wengi wa soka wanakiri kuwa makali ya Baleke ya kukaa kwenye nafasi sahihi na kumalizia pasi za mwisho yamebaki kuwa alama ya kipekee.

Kauli ya Beleke imeungwa mkono na baadhi ya mashabiki lakini wengine wamemkosoa wakidai kuwa kauli yake ni ya kujikuza tu, hasa kwa kuzingatia kuwa kwa sasa hana timu rasmi anayoichezea tangu aachane na majukumu yake ya mwisho nchini.

Katika dirisha lililopita Simba iliwasajili washambuliaji Ibrahim Doumbia na Juma Mgunda hata hivyo wawili hao wamekosa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha Simba kocha mkuu wa timu hiyo Steve barker akitegemea zaidi viungo wake washambuliaji kufunga mabao.

Aidha Barker amelazimika kumbadilishia majukumu Elie Mpanzu ambaye tangu kupewa majukumu mapya ya ushambuliaji wa kati amekuwa mwiba kwa timu pinzani akiwa amepachika mabao manne kwenye ligi mpaka sasa.

ADVERTISE HERE

More Stories

UEFA Champions League kuendelea leo kwa mechi tisa za kibabe
UEFA Champions League kuendelea leo kwa mechi tisa za kibabe
1h ago
READ MORE β†’
Barcelona na Arsenal zatamba Bayern ikiambulia sare katika usiku wa Uefa.
Barcelona na Arsenal zatamba Bayern ikiambulia sare katika usiku wa Uefa.
2h ago
READ MORE β†’
Zanzibar yafungua milango ya vipaji vya vijana kupitia Real madrid foundation
Zanzibar yafungua milango ya vipaji vya vijana kupitia Real madrid foundation
2h ago
READ MORE β†’
Keffe D ahukumiwa kifungo cha miaka 40 hadi maisha mauaji ya Tupac
Keffe D ahukumiwa kifungo cha miaka 40 hadi maisha mauaji ya Tupac
6h ago
READ MORE β†’
Simba yaichakaza Mashujaa 6-1, Mpanzu atupia mawili.
Simba yaichakaza Mashujaa 6-1, Mpanzu atupia mawili.
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Simba 6-1 Mashujaa Fc
Highlights : Simba 6-1 Mashujaa Fc
17h ago
READ MORE β†’
Ally Kamwe awaomba Wanayanga subira, asema maoni yao yatafanyiwa kazi
Ally Kamwe awaomba Wanayanga subira, asema maoni yao yatafanyiwa kazi
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yapata pigo, Abuya nje wiki mbili hadi tatu
Yanga yapata pigo, Abuya nje wiki mbili hadi tatu
1d ago
READ MORE β†’
Israel Mwenda karibu kurejea Yanga baada ya Kutatuliwa kwa sakata lake
Israel Mwenda karibu kurejea Yanga baada ya Kutatuliwa kwa sakata lake
1d ago
READ MORE β†’
Kipigo cha Simba si mwisho, lengo letu ni Ubingwa: Ally Kamwe
Kipigo cha Simba si mwisho, lengo letu ni Ubingwa: Ally Kamwe
1d ago
READ MORE β†’