Kaimu Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Yahya Abushehe, amesema Bodi hiyo imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa soka pamoja na klabu kuhakikisha kanuni na taratibu zinafuatwa kuelekea mchezo wa Kariakoo Derby.
Abushehe amesema wamekuwa wakifanya vikao na wadau mbalimbali wanaohusika na mchezo huo kwa lengo la kukumbushana wajibu na kuhakikisha kila upande unazingatia taratibu zilizowekwa.
Amesema TPLB pia inaendelea kushirikiana na Simba SC, ambao ni wenyeji wa mchezo huo, ili kuhakikisha maandalizi yanafanyika kwa umakini na kila jambo linakwenda sawa kuelekea siku ya mchezo.
βNi sehemu mojawapo ya kuendelea kukumbushana,β amesema Abushehe.
Ameongeza kuwa ushirikiano huo ni sehemu muhimu ya maandalizi, kwa lengo la kuhakikisha mchezo unafanyika katika mazingira salama, tulivu na yanayozingatia kanuni za soka.