Baada ya kupisha kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kwa ajili ya mechi za timu za taifa, Ligi Kuu ya NBC inarejea rasmi leo Alhamisi, Oktoba 8, 2026, kwa kishindo kikuu huku michezo mitatu ya kukata na shoka ikitarajiwa kupigwa katika viwanja mbalimbali nchini.
Macho ya wapenzi wa soka yataelekezwa mikoani ambapo timu zinapigania kujinasua katika nafasi za chini na zingine zikitafuta namna ya kujiweka vizuri kwenye msimamo wa ligi hiyo inayozidi kuwa ngumu kila kukicha.
Mtanange wa mapema utazikutanisha Mashujaa FC na Polisi Tanzania katika Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma majira ya saa 8:00 mchana.
Mashujaa wataingia uwanjani wakiwa na faida ya nyumbani wakijaribu kutumia vyema ngome yao, huku Polisi Tanzania wakisaka alama tatu muhimu ugenini ili kuendeleza mwanzo wao mzuri msimu huu.
Huko jijini Mwanza, miamba ya Kanda ya Ziwa, Pamba Jiji, watakuwa wenyeji wa Geita Gold katika dabi ya kukata na shoka itakayopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba majira ya saa 10:15 jioni.
Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na historia na upinzani wa jadi uliopo baina ya timu hizi mbili za kanda hiyo.
Kuhitimisha ratiba ya leo, Namungo FC watavaana na TRA United kwenye Uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa, Lindi, majira ya saa 12:30 jioni.
Namungo watahitaji kutumia vyema uwanja wao wa nyumbani kupata matokeo mbele ya TRA United ambayo ni kama wamejipata baada ya mabadiliko ya benchi la ufundi Hemed Suleiman 'Morocco' akichukua nafasi ya Etienne Ndayiragije