Kamati ya Sheria ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemwamuru beki wa kulia wa Yanga SC, Israel Patrick Mwenda, kurejea kazini na kuendelea kuheshimu masharti ya mkataba wake na klabu hiyo.
Mwenda aliwakilishwa na SPATA katika shauri hilo, huku Kamati ya Sheria ya TFF ikitoa maelekezo ya kurejea kwenye majukumu yake ndani ya klabu na kutekeleza mkataba alionao.
Kwa upande wake, Yanga SC imeendelea kusisitiza msimamo wake kwamba mchezaji huyo anapaswa kuheshimu mkataba wake na klabu, huku suala hilo likiendelea kufuatiliwa kwa mujibu wa taratibu za kisheria na kimichezo.
ADVERTISE HERE