Msemaji wa Simba, Ahmed Ally, amesema kikosi hicho kinatarajiwa kurejea kesho kutoka Afrika Kusini baada ya kuweka kambi ya siku kadhaa kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.
Ahmed Ally amesema Simba ilitumia kambi hiyo kucheza mechi mbili za kirafiki, ambazo zote ilipoteza, lakini matokeo hayo yamewasaidia kubaini maeneo yaliyohitaji maboresho kabla ya kuanza kwa ushindani rasmi.
“Timu yetu itarejea kesho kutoka South Africa ambapo tuliweka kambi ya siku kadhaa. Tumefurahi kufungwa katika mechi zote mbili za kirafiki tulizocheza.
Tumejua wapi tumekosea na kocha Steve Barker ana siku tano za kufanya masahihisho,” amesema Ahmed Ally.
Simba sasa inarejea Tanzania ikiwa na muda mfupi wa kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika michezo hiyo ya kirafiki, huku benchi la ufundi likipewa siku tano za kufanya marekebisho.