Kuelekea Derby ya Kariakoo ya Oktoba 10, tunakumbushia historia ya moja ya mechi kubwa zaidi katika soka la Tanzania na rekodi ya kipekee iliyowekwa na Simba SC.
Abdallah Athumani Seif, maarufu kama King Abdallah Kibadeni Mputa, ndiye mchezaji pekee katika historia aliyewahi kufunga hat-trick kwenye Kariakoo Derby.
Kibadeni aliandika historia hiyo Julai 19, 1977, wakati Simba ilipoichapa Yanga kwa mabao 6-0 katika pambano la 11 tangu timu hizo kuanza kukutana kwenye ligi iliyoasisiwa mwaka 1965.
Hadi leo, rekodi hiyo ya Kibadeni bado inasimama kama moja ya sura kubwa katika historia ya Derby ya Kariakoo.