Ronaldo Aondoka, wafuasi milioni 8 zapotea Ureno, nini kinaendelea nyuma ya pazia?

Jairo Mtitu By Jairo Mtitu
β€’
2h ago
Ronaldo Aondoka, wafuasi milioni 8 zapotea Ureno, nini kinaendelea nyuma ya pazia?

Kuondoka kwa Cristiano Ronaldo kwenye kambi ya timu ya taifa ya Ureno kumeibua mjadala mwingine mkubwa nje ya uwanja, baada ya akaunti rasmi ya timu hiyo kuripotiwa kupoteza mamilioni ya followers ndani ya muda mfupi.

Kwa mujibu wa takwimu zinazosambaa, akaunti hiyo ilikuwa na takribani followers milioni 32.4, kabla ya kushuka hadi karibu milioni 24.6 baada ya Ronaldo kuondoka  tofauti ya takribani milioni 7.8.

Lakini nyuma ya namba hizo kuna swali kubwa zaidi: Je, mashabiki walikuwa wanaifuatilia timu ya Ureno, au walikuwa wakimfuatilia Ronaldo?

Ronaldo ni mmoja wa watu wenye wafuasi wengi zaidi duniani kwenye mitandao ya kijamii, hivyo uwepo wake kwenye timu ya taifa una athari kubwa katika mvuto wa chapa ya Ureno.

Hata hivyo, takwimu hizi zinahitaji uthibitisho huru kabla ya kuhitimisha kwamba kuondoka kwa Ronaldo ndiko kulikosababisha kupungua huko.

Mabadiliko ya followers yanaweza pia kusababishwa na kusafishwa kwa akaunti bandia, mabadiliko ya mfumo wa jukwaa au sababu nyingine za kiufundi.

Iwapo idadi hiyo itathibitishwa, tukio hili linaweza kutoa picha ya kuvutia kuhusu nguvu ya Ronaldo kama chapa binafsi na namna anavyoweza kuathiri mvuto wa timu ya taifa hata akiwa nje ya uwanja.

More Stories

Ghana yamfuta kazi Queiroz baada ya kufungwa mechi mbili kufuzu Afcon 2027
Ghana yamfuta kazi Queiroz baada ya kufungwa mechi mbili kufuzu Afcon 2027
2h ago
READ MORE β†’
Takwimu za kiungo wa boli Duke Abuya akiingia Derby ya Kariakoo Oktoba 10
Takwimu za kiungo wa boli Duke Abuya akiingia Derby ya Kariakoo Oktoba 10
2h ago
READ MORE β†’
Simba kujipima na Timu za Afrika kusini, ikijiandaa na muendelezo wa msimu 2026-27
Simba kujipima na Timu za Afrika kusini, ikijiandaa na muendelezo wa msimu 2026-27
2h ago
READ MORE β†’
Messi kupewa shahada ya juu ya heshima na Chuo Kikuu cha Buenos Aires.
Messi kupewa shahada ya juu ya heshima na Chuo Kikuu cha Buenos Aires.
6h ago
READ MORE β†’
Ronaldo alihisi kudharauliwa kabla ya kuondoka Portugal, wachambuzi wafunguka.
Ronaldo alihisi kudharauliwa kabla ya kuondoka Portugal, wachambuzi wafunguka.
6h ago
READ MORE β†’
AS FAR kukutana na Taifa Stars kwenye mchezo wa kirafiki.
AS FAR kukutana na Taifa Stars kwenye mchezo wa kirafiki.
7h ago
READ MORE β†’
Ronaldo aondoka kambini Portugal
Ronaldo aondoka kambini Portugal
17h ago
READ MORE β†’
Simba Queens yaitandika Yanga princess 3-0 na kutinga fainali Ngao ya jamii
Simba Queens yaitandika Yanga princess 3-0 na kutinga fainali Ngao ya jamii
20h ago
READ MORE β†’
Pep Guardiola awaunga mkono Manchester city baada ya uamuzi wa ligi kuu: Tutapita pamoja
Pep Guardiola awaunga mkono Manchester city baada ya uamuzi wa ligi kuu: Tutapita pamoja
1d ago
READ MORE β†’
Mwamnyeto afunguka uhusiano wake na Diarra, Tunawasiliana muda mwingi
Mwamnyeto afunguka uhusiano wake na Diarra, Tunawasiliana muda mwingi
1d ago
READ MORE β†’