Shabiki maarufu wa Yanga, Mzee Mpili, afariki dunia

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
β€’
2d ago
Shabiki maarufu wa Yanga, Mzee Mpili, afariki dunia

Shabiki maarufu na mwanachama wa Young Africans Sports Club, Haji Omari Ramadhani Mpili, maarufu kama Mzee Mpili, amefariki dunia usiku wa Septemba 27, 2026, huko Ikwiriri, Wilaya ya Rufiji, Mkoa wa Pwani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa Yanga, Mzee Mpili alifariki katika Kituo cha Afya cha Wilaya ya Ikwiriri, alipokuwa akipatiwa matibabu. Taarifa kutoka kwa waliokuwa wakimfahamu zinaeleza kuwa alikuwa akisumbuliwa na changamoto mbalimbali za kiafya ikiwemo maumivu ya mgongo na kiuno pamoja na matatizo yanayohusiana na uzee.

Mzee Mpili alikuwa akifahamika miongoni mwa mashabiki wa Yanga kwa mapenzi yake kwa klabu hiyo, huku kifo chake kikisababisha huzuni kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na familia kubwa ya wana-Yanga.

Mazishi yake yanatarajiwa kufanyika leo Jumatatu, Septemba 28, 2026, saa 10:00 jioni katika Makaburi ya Msikiti Mkuu, Ikwiriri, Mkoa wa Pwani.

Uongozi wa Yanga umetoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wadau wa soka walioguswa na msiba huo, huku ukiwataka kuwa na subira na utulivu katika kipindi hiki kigumu.

Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Haji Omari Ramadhani Mpili mahali pema peponi na awape subira wafiwa. Amina. 

More Stories

Simba queens yaitandika Yanga princess 3-0 na kutinga fainali Ngao ya jamii
Simba queens yaitandika Yanga princess 3-0 na kutinga fainali Ngao ya jamii
7m ago
READ MORE β†’
Pep Guardiola awaunga mkono Manchester city baada ya uamuzi wa ligi kuu: Tutapita pamoja
Pep Guardiola awaunga mkono Manchester city baada ya uamuzi wa ligi kuu: Tutapita pamoja
5h ago
READ MORE β†’
Mwamnyeto afunguka uhusiano wake na Diarra, Tunawasiliana muda mwingi
Mwamnyeto afunguka uhusiano wake na Diarra, Tunawasiliana muda mwingi
7h ago
READ MORE β†’
Kagera sugar yaongeza wazawa benchi la ufundi, Kiemba na Domayo waingia kuungana na Kaze
Kagera sugar yaongeza wazawa benchi la ufundi, Kiemba na Domayo waingia kuungana na Kaze
8h ago
READ MORE β†’
Israel Mwenda apeleka sakata lake Spata, mazungumzo na Yanga yaanza
Israel Mwenda apeleka sakata lake Spata, mazungumzo na Yanga yaanza
9h ago
READ MORE β†’
Wallace Karia Kukutana na Vilabu vya Ligi Kuu ya Wanawake
Wallace Karia Kukutana na Vilabu vya Ligi Kuu ya Wanawake
11h ago
READ MORE β†’
Fabrice Shema Ajiuzulu Urais wa FERWAFA
Fabrice Shema Ajiuzulu Urais wa FERWAFA
12h ago
READ MORE β†’
Yanga warejea mazoezini, Maandalizi ya mechi zijazo yakianza
Yanga warejea mazoezini, Maandalizi ya mechi zijazo yakianza
23h ago
READ MORE β†’
Manchester city yapinga mashtaka yanayowakabili, ikipanga kuchukua hatua
Manchester city yapinga mashtaka yanayowakabili, ikipanga kuchukua hatua
1d ago
READ MORE β†’
Makonda awaitisha viongozi wa Simba SC.
Makonda awaitisha viongozi wa Simba SC.
1d ago
READ MORE β†’