Salah hakamatiki Uturuki, apiga hat-trik Trabzonspor ikiifumua Galatasaray 4-0

Joel JJ By Joel JJ
β€’
20 Sep 2026
Salah hakamatiki Uturuki, apiga hat-trik Trabzonspor ikiifumua Galatasaray 4-0

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Misri, Mohamed Salah, ameonyesha kiwango cha juu nchini Uturuki baada ya kufunga hat-trick na kutoa asisti moja katika ushindi mkubwa wa Trabzonspor wa mabao 4-0 dhidi ya Galatasaray.

Katika mchezo huo wa wiki ya sita ya Ligi Kuu ya Uturuki (Trendyol Super Lig) uliochezwa Jumamosi, Septemba 19, 2026, Trabzonspor waliitawala Galatasaray na kumaliza mchezo wakiwa na ushindi mnono wa mabao manne bila majibu.

Salah aanza kwa kishindo

Salah hakusubiri muda mrefu kuonyesha madhara yake.

Dakika ya 4, nyota huyo wa Misri aliifungia Trabzonspor bao la kwanza baada ya kupokea pasi ya Mustafa Eskihellac, kabla ya kuingia kwenye eneo la hatari na kumalizia kwa ustadi.

Bao hilo liliipa Trabzonspor mwanzo mzuri na kuweka Galatasaray kwenye presha mapema.

Trabzonspor waliendelea kutawala na kupata bao la pili dakika ya 39.

Safari hii Salah hakuwa mfungaji, bali alikuwa mtoa asisti. Alimpatia Noah Saviolo mpira uliomuwezesha kufunga na kuifanya Trabzonspor kuongoza 2-0.

Hivyo, kabla hata ya mapumziko, Salah alikuwa tayari amehusika moja kwa moja katika mabao mawili ya timu yake.

Dakika chache kabla ya mapumziko, Salah aliandika bao lake la pili.

Dakika ya 44, Franculino alimpatia mpira Salah ndani ya eneo la hatari, na mshambuliaji huyo akautuliza kabla ya kuufunga kwa mkwaju wa chini.

Trabzonspor wakaenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 3-0.

Kama vile usiku huo haukuwa bado wake, Salah alimalizia kazi yake dakika ya 80.

Alipokea pasi kutoka kwa Ozan Tufan, akaingia kwenye eneo la hatari na kumalizia kwa ustadi na kuifanya Trabzonspor kuongoza 4-0.

Hilo likawa bao lake la tatu katika mchezo huo na kukamilisha hat-trick yake.

ADVERTISE HERE

More Stories

UEFA Champions League kuendelea leo, macho kuelekezwa PSG dhidi ya Barcelona
UEFA Champions League kuendelea leo, macho kuelekezwa PSG dhidi ya Barcelona
46m ago
READ MORE β†’
CAF yabadilisha mwamuzi wa mchezo wa Simba SC dhidi ya 15 de Agosto
CAF yabadilisha mwamuzi wa mchezo wa Simba SC dhidi ya 15 de Agosto
22h ago
READ MORE β†’
Kocha wa Wiliete SC alazwa hospitalini baada ya mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns
Kocha wa Wiliete SC alazwa hospitalini baada ya mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns
22h ago
READ MORE β†’
TFF kuja na zoezi la upimaji wa dawa zilizokatazwa kwa wachezaji
TFF kuja na zoezi la upimaji wa dawa zilizokatazwa kwa wachezaji
22h ago
READ MORE β†’
Azam FC yawasha moto, yaanza maandalizi kuivunja ZED FC Chamazi
Azam FC yawasha moto, yaanza maandalizi kuivunja ZED FC Chamazi
22h ago
READ MORE β†’
Simba kuweka big screen Mwembe Yanga, mashabiki watakiwa kuvaa jezi mpya
Simba kuweka big screen Mwembe Yanga, mashabiki watakiwa kuvaa jezi mpya
23h ago
READ MORE β†’
Rangers yaelekea Caf kufuatia vurugu za mashabiki wa Mc Alger
Rangers yaelekea Caf kufuatia vurugu za mashabiki wa Mc Alger
1d ago
READ MORE β†’
Saido Berahino astaafu soka la ushindani akiwa na umri wa miaka 33
Saido Berahino astaafu soka la ushindani akiwa na umri wa miaka 33
1d ago
READ MORE β†’
Kutoka bodaboda Iringa hadi kuwa nyota wa Yanga SC - Clement Mzize:
Kutoka bodaboda Iringa hadi kuwa nyota wa Yanga SC - Clement Mzize:
1d ago
READ MORE β†’
Waziri Makonda afichua mpango wa kujenga Arena tatu za kisasa za michezo
Waziri Makonda afichua mpango wa kujenga Arena tatu za kisasa za michezo
1d ago
READ MORE β†’