Local, Transfer News, Azam Fc, Yanga, Simba

Fei Toto azipotezea Simba, Yanga

Joel JJ By Joel JJ
β€’
11h ago
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga

Kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’, ameendelea kuwa kimya kuhusu tetesi zinazomhusisha na vigogo wa soka la Tanzania, Simba na Yanga, akisisitiza kuwa kwa sasa bado ana mkataba na Azam FC na hana haraka ya kuzungumzia kinachoweza kutokea baadae.

Mustakabali wa Fei Toto umeendelea kuwa gumzo kutokana na ubora wake pamoja na ukweli kwamba mkataba wake na Azam FC unatarajiwa kufikia mwisho Juni 2027.

Hata hivyo, mchezaji huyo amegoma kuingia kwenye mjadala wa mapema kuhusu klabu atakayochezea baada ya mkataba wake kumalizika.

Fei Toto amekuwa akihusishwa na Simba na Yanga katika kipindi cha usajili, lakini alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kuhamia moja ya klabu hizo, Fei Toto alisema yeye anaweza kuitumikia timu yoyote ambayo itakidhi maslahi yake.

Aidha nyota huyo pia akaweka wazi kuwa yeye sio mchezaji wa kuwa na mapenzi na timu kwa sababu mpira wa miguu ndio kazi yake na lazima awe tayari kuitumikia timu yoyote.

Muda wake bado haujafika

Fei Toto ametaka suala la hatima yake libaki pembeni kwa sasa, akieleza kuwa bado hajafikia hatua ambayo kanuni zinamruhusu kuanza mazungumzo rasmi na klabu nyingine.

Kiungo huyo fundi amesema, kipindi cha miezi sita ya mwisho ya mkataba ndicho kitakachokuwa muhimu zaidi iwapo kutakuwa na hatua mpya kuhusu mustakabali wake.

Azam bado ni kipaumbele

Fei Toto amesisitiza kuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Azam FC kinacholenga kupambana kwa ajili ya ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Kiungo huyo amesisitiza umuhimu wa timu yake kukusanya matokeo katika kila mchezo, hasa baada ya Azam kukumbana na sare katika baadhi ya mechi za mwanzo wa msimu.

Msimu uliopita Azam Fc ilimaliza katika nafasi ya tatu, huku sare nyingi zikiwa miongoni mwa mambo yaliyowagharimu katika mbio za ubingwa. Fei Toto anaamini hali hiyo haipaswi kujirudia ikiwa timu hiyo inataka kuwa tishio kubwa kwenye mbio za kutwaa taji msimu huu.

Mashabiki bado wana nafasi muhimu

Mbali na kuzungumzia malengo ya timu, Fei Toto amewataka mashabiki wa Azam FC kuendelea kujitokeza kwa wingi katika michezo ya timu hiyo.

Anaamini uwepo na hamasa ya mashabiki unaweza kuwapa wachezaji nguvu zaidi wanapokuwa ndani ya uwanja, hasa katika kipindi ambacho timu inapambana kujenga mwendelezo mzuri wa matokeo.

More Stories

Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
2h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
4h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
6h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
8h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
8h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
9h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
14h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
21h ago
READ MORE β†’
Wapinzani wa Simba, Mighty Wanderers kutua nchini leo wakitokea Malawi
Wapinzani wa Simba, Mighty Wanderers kutua nchini leo wakitokea Malawi
1d ago
READ MORE β†’