Local, Transfer News, TRA United

Morocco apindua meza TRA United, kumrithi Ndayirajige

Joel JJ By Joel JJ
β€’
2d ago
Morocco apindua meza TRA United, kumrithi Ndayirajige

Klabu ya TRA United inatajwa kumteua kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Hemed Suleiman (56), kuwa kocha mpya wa timu hiyo, akichukua nafasi ya Etienne Ndayiragije ambaye alitimuliwa siku chache zilizopita.

Hemed anarejea kwenye soka la ushindani akiwa na jukumu la kuiongoza TRA United katika kipindi ambacho timu hiyo inatafuta mwendelezo mzuri wa matokeo.

Ujio wa Hemed unafuatia taarifa za awali zilizohusisha TRA United na kocha wa zamani wa Mbeya City, Meckie Mexime, ambaye inadaiwa alisimamia mazoezi ya timu hiyo siku ya Jumanne wakati klabu ikiwa katika mchakato wa kumpata kocha mpya.

Hata hivyo, TRA United imeamua kumpa nafasi Hemed, ambaye ana uzoefu mkubwa katika soka la Tanzania, ikiwemo kipindi alichokuwa sehemu ya benchi la ufundi la Taifa Stars.

Kocha huyo sasa anakabiliwa na jukumu la kuijenga upya TRA United na kuhakikisha timu hiyo inapata matokeo yatakayoiweka kwenye nafasi nzuri baada ya kuanza kwa kuchechea katika msimu huu.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
5h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
8h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
10h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
12h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
14h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
15h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
15h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
17h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
20h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’