Simba yapanga kusafiri na mashabiki Malawi, Ligi ya Mabingwa

Joel JJ By Joel JJ
β€’
24 Aug 2026
Simba yapanga kusafiri na mashabiki Malawi, Ligi ya Mabingwa

Simba SC imeandaa mpango maalum wa kusafiri na mashabiki wake kwenda Malawi wakati timu hiyo ikianza kampeni za Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) msimu wa 2026/27.

Simba itaanza safari yake ya kimataifa kwa kukutana na Mighty Wanderers ya Malawi katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya awali, unaotarajiwa kuchezwa Septemba 6, 2026, nchini Malawi.

Mchezo wa marudiano umepangwa kufanyika Septemba 13, 2026, jijini Dar es Salaam, huku Simba ikitarajiwa kutangaza uwanja utakaotumika baadaye.

Simba kusafiri na mashabiki Malawi

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema klabu hiyo imeandaa basi maalum litakalowapeleka mashabiki Malawi ili kuipa timu sapoti ya kutosha katika mchezo huo muhimu wa kimataifa.

Kwa mujibu wa Ahmed, safari ya mashabiki itaanza Septemba 3, 2026, saa 1:00 usiku kutoka Dar es Salaam kuelekea Lilongwe, Malawi. Mashabiki watakusanyika Ubungo katika kituo cha Engen kabla ya kuanza safari.

Simba inalenga kuwa na angalau mabasi matatu kwa ajili ya mashabiki, huku safari hiyo ikielezwa kuwa ya kifahari na yenye lengo la kuwapa mashabiki nafasi ya kuisindikiza timu yao katika hatua hii ya michuano.

“Kwa kuwa tunakwenda Malawi, tumeandaa safari ya basi la mashabiki kwenda Malawi. Tumeshawahi kusafiri huko nyuma kwa basi kwenda Malawi, Zambia na hata Uganda. Safari hii tunakwenda kucheza na Mighty Wanderers tukasema tusiiache timu iende peke yake,” alisema Ahmed Ally.

Akaongeza: “Safari hii tunarejea tena Malawi na safari hii tunataka kuvunja rekodi ya kusafiri na mashabiki wengi.”

Passport ni sharti kwa mashabiki

Mashabiki wanaopanga kusafiri wameelekezwa kuwa na hati halali ya kusafiria. Ahmed Ally amesema sharti hilo litazingatiwa ili kuepusha usumbufu wakati wa safari.

“Kama unataka kwenda Malawi sharti la kwanza uwe na hati ya kusafiria (passport). Kama huna basi anza hata mchakato wa kutafuta ile ya karatasi, Malawi wanaruhusu pia ile ya karatasi. Kuepusha usumbufu, hatapanda mtu ambaye hana passport,” alisema.

Mashabiki wanaotaka kuweka nafasi ya safari hiyo wametakiwa kupiga simu kupitia namba 0742-771311 kwa ajili ya oda na kupata maelezo zaidi kuhusu safari.

Simba kuanza safari ya CAFCL kwa hamasa

Safari hiyo ya mashabiki inakuja wakati Simba ikijiandaa kurejea katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa na malengo makubwa ya kufanya vizuri zaidi msimu huu.

Ahmed Ally amesema klabu imefanya tathmini ya msimu uliopita na kuchukua hatua mbalimbali, ikiwemo kusajili wachezaji wenye uzoefu mkubwa, ili kuimarisha kikosi kwa ajili ya mashindano ya kimataifa.

“Ya mwaka jana yalishapita, tulifanya uchambuzi wa kutosha, tumesajili wachezaji wakubwa na wenye uzoefu mkubwa. Ni imani yetu mwaka huu tutavuka hatua ya makundi na kwenda robo fainali,” alisema Ahmed.

Simba imeweka wazi kuwa haitaki kuishia katika hatua za awali au makundi pekee, bali inalenga kufika mbali zaidi katika mashindano hayo. Kwa mujibu wa Ahmed, lengo kubwa la klabu msimu huu ni kufika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hivyo, mchezo dhidi ya Mighty Wanderers utakuwa mwanzo wa safari hiyo, huku Simba ikitarajia kupata matokeo mazuri nchini Malawi kabla ya mchezo wa marudiano Septemba 13, 2026, Dar es Salaam.

ADVERTISE HERE

More Stories

Ronaldo bado mabao 20 tu afikishe 1000
Ronaldo bado mabao 20 tu afikishe 1000
9m ago
READ MORE β†’
Gas Detectors kutumika Kariakoo Derby
Gas Detectors kutumika Kariakoo Derby
3h ago
READ MORE β†’
Highlights : Coastal Union 0-2 Azam Fc
Highlights : Coastal Union 0-2 Azam Fc
11h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaizamisha Coastal Union kwa mabao 2-0
Azam FC yaizamisha Coastal Union kwa mabao 2-0
11h ago
READ MORE β†’
CFFA yairahisishia kazi Yanga Ligi ya Mabingwa
CFFA yairahisishia kazi Yanga Ligi ya Mabingwa
18h ago
READ MORE β†’
JKT Tanzania yaichapa Fountain Gate 2-1
JKT Tanzania yaichapa Fountain Gate 2-1
18h ago
READ MORE β†’
Tupo tayari kupambana na kupata matokeo dhidi ya Yanga: Neo Maema
Tupo tayari kupambana na kupata matokeo dhidi ya Yanga: Neo Maema
22h ago
READ MORE β†’
Steve Barker azungumzia ubora wa Yanga kuelekea Kariakoo Derby
Steve Barker azungumzia ubora wa Yanga kuelekea Kariakoo Derby
22h ago
READ MORE β†’
Yanga tumejipanga vizuri kuikabili Simba - Manqoba Mngqithi
Yanga tumejipanga vizuri kuikabili Simba - Manqoba Mngqithi
22h ago
READ MORE β†’
Ahmed Arajiga kuchezesha dabi ya Simba na Yanga kesho
Ahmed Arajiga kuchezesha dabi ya Simba na Yanga kesho
23h ago
READ MORE β†’