Local, Transfer News, Tetesi, Simba, JKT Tanzania

Simba yakwama kwa Paul Peter

Joel JJ By Joel JJ
β€’
15 Aug 2026
Simba yakwama kwa Paul Peter

Klabu ya Simba SC imeshindwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji Paul Peter Kasunda kutoka JKT Tanzania, baada ya muda wa kukamilisha uhamisho huo kuisha.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, JKT Tanzania ilikuwa imeitaka Simba kukamilisha usajili wa mshambuliaji huyo kabla ya saa 12 jioni, ili kutoa nafasi kwa klabu hiyo ya kijeshi kupata muda wa kutafuta na kumsajili mbadala wake.

Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa Simba iliwasiliana na JKT Tanzania majira ya saa 4 usiku, wakati ambapo muda wa usajili ulikuwa umekwisha na maafande hao tayari walikuwa wameamua kusitisha uhamisho huo kutokana na ufinyu wa muda wa kupata mbadala wa Kasunda.

Inaelezwa pia kuwa kulikuwa na mvutano ndani ya uongozi wa Simba kuhusu usajili wa mshambuliaji huyo, huku baadhi ya viongozi wakipinga hatua hiyo, hasa baada ya klabu hiyo kumsajili Ismail Mgunda.

Katika hatua nyingine, kulikuwa na mapendekezo ndani ya Simba ya kusajili mshambuliaji wa kigeni au kiungo mkabaji, lakini mipango hiyo nayo haikuweza kutekelezwa.

Kwa sasa, Simba imefunga dirisha lake la usajili kwa kuwaongeza kikosini Ismail Mgunda pamoja na beki Ibrahim Nindi. Aidha, mpango wa kumsajili kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ pia haukufanikiwa.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’