Simba, Mgunda makubaliano yamefikiwa, asubiri utambulisho

Joel JJ By Joel JJ
β€’
12 Aug 2026
Simba, Mgunda makubaliano yamefikiwa, asubiri utambulisho

Klabu ya Simba SC imefikia makubaliano na Mashujaa FC juu ya uhamisho wa mshambuliaji Ismail Mgunda, ambaye anatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kukamilisha hatua za mwisho za kujiunga na Wekundu wa Msimbazi.

Mgunda anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji wapya watakaoiongezea nguvu Simba katika safu ya ushambuliaji, baada ya klabu hiyo kufikia makubaliano na Mashujaa FC juu ya mauziano ya mshambuliaji huyo.

Taarifa zinaeleza kuwa Mgunda alishiriki katika mazoezi ya mwisho na Mashujaa FC jana, kabla ya kupewa ruhusa na klabu hiyo kusafiri kuelekea Dar es Salaam leo kwa ajili ya kukamilisha uhamisho wake.

Mshambuliaji huyo alikuwa sehemu ya kikosi cha Mashujaa FC kilichoweka kambi ya maandalizi ya msimu jijini Tanga, akishiriki kikamilifu katika programu ya maandalizi ya timu hiyo kuelekea msimu mpya.

Baada ya kuwasili Dar es Salaam, Mgunda anatarajiwa kukamilisha taratibu za mwisho za usajili kabla ya kusubiri utambulisho rasmi wa Simba.

Kwa mujibu wa taarifa, mshambuliaji huyo anatarajiwa kuungana na kikosi cha Simba baada ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga utakaopigwa leo katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Usajili wa Mgunda unatajwa kuwa mbadala wa mshambuliaji Suleiman Mwalimu ambaye jana aliwa-sapraizi Simba kwa kujiunga na watani zao wa jadi, Yanga.

ADVERTISE HERE

More Stories

CAF yabadilisha mwamuzi wa mchezo wa Simba SC dhidi ya 15 de Agosto
CAF yabadilisha mwamuzi wa mchezo wa Simba SC dhidi ya 15 de Agosto
7m ago
READ MORE β†’
Kocha wa Wiliete SC alazwa hospitalini baada ya mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns
Kocha wa Wiliete SC alazwa hospitalini baada ya mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns
40m ago
READ MORE β†’
TFF kuja na zoezi la upimaji wa dawa zilizokatazwa kwa wachezaji
TFF kuja na zoezi la upimaji wa dawa zilizokatazwa kwa wachezaji
44m ago
READ MORE β†’
Azam FC yawasha moto, yaanza maandalizi kuivunja ZED FC Chamazi
Azam FC yawasha moto, yaanza maandalizi kuivunja ZED FC Chamazi
56m ago
READ MORE β†’
Simba kuweka big screen Mwembe Yanga, mashabiki watakiwa kuvaa jezi mpya
Simba kuweka big screen Mwembe Yanga, mashabiki watakiwa kuvaa jezi mpya
1h ago
READ MORE β†’
Rangers yaelekea Caf kufuatia vurugu za mashabiki wa Mc Alger
Rangers yaelekea Caf kufuatia vurugu za mashabiki wa Mc Alger
3h ago
READ MORE β†’
Saido Berahino astaafu soka la ushindani akiwa na umri wa miaka 33
Saido Berahino astaafu soka la ushindani akiwa na umri wa miaka 33
4h ago
READ MORE β†’
kutoka bodaboda Iringa hadi kuwa nyota wa Yanga SC - Clement Mzize:
kutoka bodaboda Iringa hadi kuwa nyota wa Yanga SC - Clement Mzize:
4h ago
READ MORE β†’
Waziri Makonda afichua mpango wa kujenga Arena tatu za kisasa za michezo
Waziri Makonda afichua mpango wa kujenga Arena tatu za kisasa za michezo
8h ago
READ MORE β†’
Ndejembi atamani kuziona Simba na Yanga kwenye mpira wa kikapu
Ndejembi atamani kuziona Simba na Yanga kwenye mpira wa kikapu
8h ago
READ MORE β†’