Senegal yapigika 3-1 mbele ya Ufaransa

Joel JJ By Joel JJ
•
17 Jun 2026
Senegal yapigika 3-1 mbele ya Ufaransa

Ufaransa imeanza kampeni yake ya Kombe la Dunia 2026 kwa ushindi muhimu wa mabao 3-1 dhidi ya Senegal katika mchezo wa Kundi I uliochezwa Jumanne nchini Marekani.

Nahodha wa Ufaransa, Kylian Mbappé, alikuwa shujaa wa mechi hiyo baada ya kufunga mabao mawili yaliyoiwezesha timu yake kuondoka na alama tatu muhimu. Ushindi huo umeiweka Ufaransa katika nafasi nzuri ya kuwania kufuzu hatua ya mtoano mapema.

Licha ya matokeo hayo, Senegal ndiyo iliyotawala sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza. Washambuliaji wake walitengeneza nafasi kadhaa za wazi kupitia Sadio Mané, Nicolas Jackson na Ismaïla Sarr, lakini walishindwa kuzitumia ipasavyo mbele ya lango la Ufaransa.

Baada ya mapumziko, Ufaransa ilirejea uwanjani ikiwa na kasi mpya. Mbappé ulifungua akaunti yake ya mabao dakika ya 66 baada ya kumalizia vizuri pasi ya Michael Olise. Bao hilo lilifungua mchezo na kuwapa Wafaransa kujiamini zaidi katika mashambulizi yao.

Dakika ya 82, Bradley Barcola aliifungia Ufaransa bao la pili na kuonekana kuhitimisha mchezo. Hata hivyo, Senegal haikukata tamaa na kufanikiwa kupunguza pengo kupitia Ibrahim Mbaye katika dakika za mwisho za muda wa nyongeza.

Lakini matumaini ya Senegal yalidumu kwa muda mfupi tu. Mbappé alifunga bao la tatu kwa shuti kali la mbali muda mfupi baadaye na kuhitimisha ushindi wa 3-1 kwa mabingwa hao wa dunia wa mwaka 2018.

Mbali na kuipa Ufaransa ushindi, mabao hayo mawili yamemfanya Mbappé kuwa mfungaji bora wa muda wote katika historia ya timu ya taifa ya Ufaransa akiwa na mabao 58, akimpita Olivier Giroud. Pia amefikisha mabao 14 katika historia ya Kombe la Dunia, akijiweka miongoni mwa wafungaji wakubwa zaidi wa mashindano hayo.

Kwa matokeo hayo, Ufaransa inaongoza mbio za kufuzu kutoka Kundi I huku Senegal ikilazimika kutafuta matokeo mazuri katika michezo yake ijayo dhidi ya Norway na Iraq ili kuendelea kuwa na matumaini ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

ADVERTISE HERE

More Stories

De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
5h ago
READ MORE →
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
7h ago
READ MORE →
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
7h ago
READ MORE →
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
8h ago
READ MORE →
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
9h ago
READ MORE →
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
10h ago
READ MORE →
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
12h ago
READ MORE →
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
14h ago
READ MORE →
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
15h ago
READ MORE →
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
16h ago
READ MORE →