Misri, Cape Verde kuwakabili vigogo kombe la Dunia leo

Joel JJ By Joel JJ
β€’
15 Jun 2026
Misri, Cape Verde kuwakabili vigogo kombe la Dunia leo

Leo Juni 15, mikiki mikiki ya Kombe la Dunia 2026 inaendelea Mexico, Canada na marekani ambapo mechi kadhaa kali zinatarajiwa kuchezwa.

Moja ya mechi zinazovuta hisia za mashabiki wengi wa soka Afrika ni ile ya Spain dhidi ya Cape Verde, ambapo mabingwa wa Ulaya wanatarajiwa kuanza kampeni yao dhidi ya timu ya Cape Verde inayoshiriki Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kabisa katika historia yake.

Huu ni mtihani mkubwa kwa Cape Verde, lakini pia ni nafasi ya kuonyesha kuwa hawakufika kimakosa. Mchezo huo utapigwa saa 1 usiku.

Kwa upande mwingine, macho ya Afrika pia yatakuwa kwenye pambano kati ya Belgium na Egypt saa 4 usiku, ambapo Misri inakutana na moja ya timu zenye wachezaji wenye uzoefu mkubwa wa ligi za Ulaya.

Misri inahitaji matokeo mazuri ili kujiweka katika mazingira bora ya kusonga mbele kwenye kundi gumu lenye ushindani mkubwa.

Mechi nyingine kubwa ni Saudi Arabia dhidi ya Uruguay, pambano linaloleta ladha ya Amerika Kusini dhidi ya Asia, huku Uruguay wakitazamiwa kutumia uzoefu wao wa mashindano ya kimataifa kukabiliana na kasi na nidhamu ya Saudi Arabia.

Pia kuna mchezo kati ya Iran na New Zealand, ambao unatarajiwa kuwa wa ushindani wa nguvu na mbinu, kila timu ikisaka pointi muhimu katika hatua za awali za makundi.

ADVERTISE HERE

More Stories

Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
2h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
4h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
5h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
5h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
7h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
7h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
7h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
20h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
1d ago
READ MORE β†’