Eriksen kufanyiwa uchunguzi zaidi baada ya tukio la kuanguka tena uwanjani

Joel JJ By Joel JJ
β€’
8 Jun 2026
Eriksen kufanyiwa uchunguzi zaidi baada ya tukio la kuanguka tena uwanjani

Christian Eriksen amewekwa chini ya uangalizi wa karibu wa kitabibu baada ya tukio la ghafla lililotokea uwanjani ambapo alionekana kuanguka na kupoteza fahamu kwa muda mfupi kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Denmark dhidi ya Ukraine uliopigwa Jumapili usiku huko Denmark

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na timu ya matibabu, Eriksen alipata huduma ya haraka uwanjani na hali yake ilianza kuimarika baada ya muda mfupi, ambapo fahamu zake zilirejea.

Taarifa zinaeleza kuwa Eriksen anaendelea vizuri na hali yake kwa ujumla iko chini ya uangalizi wa wataalamu. Vifaa vya kudhibiti mapigo ya moyo vilivyowekwa mwilini mwake vimeonyesha kufanya kazi kama ilivyokusudiwa, na hakuna dalili za tatizo kubwa la haraka lililogunduliwa wakati wa tukio hilo.

Hata hivyo, madaktari wamesisitiza kuwa atafanyiwa vipimo zaidi hospitalini ili kubaini chanzo halisi cha tukio hilo la kupoteza fahamu ghafla.

β€œSasa atafanyiwa uchunguzi zaidi hospitalini ili kubaini haswa kilichosababisha kutokea tukio hilo. Tunaendelea kuwasiliana naye pamoja na madaktari wake wa karibu hospitalini,” alisema daktari wa Denmark

Pia imeelezwa kuwa Eriksen mwenyewe amekuwa na hali nzuri ya mawasiliano baada ya tukio hilo na alituma salamu kwa wachezaji wenzake akiwahakikishia kuwa yuko sawa.

β€œIla Christian anaendelea vizuri, na aliniomba nitume salamu zake kwa wachezaji wote na kuwaambia kwamba yuko sawa.”

ADVERTISE HERE

More Stories

Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
2h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
4h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
5h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
5h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
7h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
7h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
7h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
20h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
1d ago
READ MORE β†’