Perez ataweza kumpata Olise?

Joel JJ By Joel JJ
•
6 Jun 2026
Perez ataweza kumpata Olise?

Klabu ya Real Madrid inaripotiwa kuandaa ofa kubwa ya pauni milioni 130 (zaidi ya Shilingi bilioni 455) kwa mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich, ili kumsajili winga wa kimataifa wa Ufaransa, Michael Olise.

Kwa mujibu wa taarifa za karibu na klabu hiyo, rais wa Real Madrid, Florentino Pérez, amemuweka Olise kama moja ya malengo makuu ya usajili, akiamini kuwa nyota huyo anaweza kuwa mradi mpya wa muda mrefu katika kikosi cha Santiago Bernabéu.

Inadaiwa Pérez anataka kumsajili Olise kama “zawadi ya kwanza” kwa kocha mpya au anayetarajiwa kupewa majukumu makubwa, José Mourinho, huku klabu hiyo ikiwa katika kipindi cha mabadiliko ya kisiasa kuelekea uchaguzi wa klabu unaotarajiwa kufanyika Jumapili, Juni 7, 2026.

Hata hivyo, Bayern Munich wameweka msimamo mkali kwamba nyota huyo hauzwi. Mwenyekiti wa heshima wa klabu hiyo, Uli Hoeness, ameripotiwa kusisitiza kuwa Olise ni sehemu muhimu ya mipango ya muda mrefu ya Bayern na hawana mpango wa kumuuza, badala yake wako tayari kuboresha mkataba wake na mshahara wake ili kumbakiza Allianz Arena.

Olise, ambaye bado ana mkataba hadi mwaka 2029, amekuwa na msimu bora uliojaa ubunifu, mabao na pasi za mwisho, hatua iliyomuweka miongoni mwa wachezaji waliovutia zaidi barani Ulaya. Mafanikio yake yalimfanya kutunukiwa tuzo ya Mchezaji Bora anayecheza nje ya Ufaransa, ishara ya ukuaji wake mkubwa katika soka la kimataifa.

Licha ya msimamo wa Bayern, Real Madrid wanaonekana kutokata tamaa, wakiamini kuwa ofa yao kubwa inaweza kubadilisha maamuzi ya Wajerumani. Mashabiki wa Los Blancos sasa wanasubiri kuona kama Bernabéu itampokea Olise kama mrithi wa kizazi kipya cha mastaa wa klabu hiyo.

ADVERTISE HERE

More Stories

Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
21m ago
READ MORE →
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
3h ago
READ MORE →
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
5h ago
READ MORE →
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
6h ago
READ MORE →
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
6h ago
READ MORE →
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
8h ago
READ MORE →
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
8h ago
READ MORE →
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
8h ago
READ MORE →
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
21h ago
READ MORE →
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE →