Robertison atua Spurs

Joel JJ By Joel JJ
β€’
5 Jun 2026
Robertison atua Spurs

Tottenham Hotspur wamekamilisha usajili wa beki wa kushoto wa kimataifa wa Scotland, Andy Robertson, akitokea Liverpool FC kwa uhamisho wa bure baada ya mkataba wake kumalizika.

Robertson amefikia makubaliano ya kujiunga na Spurs baada ya kipindi cha mazungumzo kilichodumu kwa miezi kadhaa, huku klabu hiyo ya London ikimwona kama nyongeza muhimu ya uzoefu katika kikosi chake.

Robertson, ambaye amekuwa mmoja wa mabeki bora wa kushoto katika Ligi Kuu England kwa zaidi ya muongo mmoja, anaondoka Liverpool baada ya kipindi cha mafanikio kilichomwona akishinda mataji makubwa ikiwemo Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Taarifa zinaeleza kuwa mchezaji huyo alikubali mradi wa Spurs kutokana na nafasi ya kuwa sehemu ya kikosi kipya chenye mwelekeo wa kujengwa upya, huku pia akipewa nafasi ya uongozi ndani ya timu.

Katika Liverpool, Robertson ameacha alama kubwa kama mmoja wa wachezaji waliobadilisha nafasi ya beki wa pembeni kuwa sehemu ya mashambulizi yenye ubunifu mkubwa, akijipatia sifa kutokana na pasi na mchango wake wa moja kwa moja kwenye mabao.

Uhamisho huo unatajwa kuwa moja ya dili kubwa za bure msimu huu barani Ulaya, ukionyesha mabadiliko ya kikosi cha Liverpool kinachoingia katika kipindi kipya baada ya misimu mingi ya mafanikio.

ADVERTISE HERE

More Stories

Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
30m ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
3h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
5h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
6h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
6h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
8h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
8h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
8h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
21h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’