PSG atinga fainali UEFA champions League, kwa mara ya pili mfululizo

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
‱
7 May 2026
PSG atinga fainali UEFA champions League, kwa mara ya pili mfululizo

Paris Saint-Germain wamefanikiwa kutinga fainali ya UEFA Champions League kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Bayern Munich na kusonga mbele kwa jumla ya mabao 6-5. Mchezo huo ulikuwa wa ushindani mkubwa huku Bayern wakijaribu kurejea katika mchezo mbele ya mashabiki wao wa nyumbani, lakini PSG walionyesha utulivu na uzoefu wa mabingwa watetezi.

Ousmane Dembélé aliifungia PSG bao muhimu kwa ustadi mkubwa, kabla ya Harry Kane kusawazisha kwa Bayern kupitia bao la dakika za mwisho lililowapa matumaini mashabiki wa Allianz Arena. Hata hivyo, juhudi hizo hazikutosha kuizuia PSG kufuzu kwenda hatua ya mwisho ya mashindano hayo makubwa barani Ulaya.

Miongoni mwa walioangaza zaidi kwa PSG alikuwa Khvicha Kvaratskhelia, ambaye alitoa kiwango cha juu kwa kutumia kasi, ubunifu na uwezo wake wa kuwatesa mabeki wa Bayern muda wote wa mchezo. Pia Willian Pacho alikuwa imara sana katika safu ya ulinzi, akizuia mashambulizi mengi ya Bayern kwa utulivu mkubwa.

Mchezo huo pia ulikuwa na utata mkubwa baada ya Nuno Mendes kuonekana kugusa mpira kwa mkono akiwa tayari ana kadi ya njano. Mashabiki wa Bayern walidai kadi ya pili, lakini waamuzi waliamua kutoa fauli dhidi ya Konrad Laimer badala yake, pamoja na hilo pia Bayern walilalamikia mpira ulioshikwa na mchezaji wa PSG, Joao neves ikionekana ni penati ya wazi licha ya waamuzi kuamua tofauti na mawazo hayo. Maamuzi hayo yaliibua malalamiko makubwa kutoka kwa upande wa Bayern huku PSG wakivuta pumzi ya afueni.

Sasa fainali ya UEFA Champions League msimu wa 2025/26 imekamilika rasmi, ambapo PSG watachuana na Arsenal FC katika dimba la Puskås Aréna mjini Budapest tarehe 30 Mei 2026. Arsenal wanakuja na ndoto ya kutwaa taji lao la kwanza Ulaya baada ya kusubiri kwa miaka 20, huku PSG wakisaka kuendeleza utawala wao kama mabingwa watetezi.

ADVERTISE HERE

More Stories

Manchester United yafanya comeback ya kusisimua, PSG ikitoa mvua ya mabao ndani ya usiku wa UEFA
Manchester United yafanya comeback ya kusisimua, PSG ikitoa mvua ya mabao ndani ya usiku wa UEFA
7h ago
READ MORE →
Mbeya City yaichapa Singida BS, yaibuka na pointi tatu
Mbeya City yaichapa Singida BS, yaibuka na pointi tatu
14h ago
READ MORE →
Singida BS yavunja mkataba na Marcel Canadi
Singida BS yavunja mkataba na Marcel Canadi
20h ago
READ MORE →
West Ham yamfuta kazi Nuno EspĂ­rito Santo
West Ham yamfuta kazi Nuno EspĂ­rito Santo
20h ago
READ MORE →
Soka laomboleza kifo cha JesĂșs de Miguel wa CD Tenerife
Soka laomboleza kifo cha JesĂșs de Miguel wa CD Tenerife
21h ago
READ MORE →
NBC Premier League kuendelea leo kwa pambano la Mbeya City na Singida BS
NBC Premier League kuendelea leo kwa pambano la Mbeya City na Singida BS
21h ago
READ MORE →
Haina kupoa..! UEFA Champions League kupigika leo kwa mechi za kibabe
Haina kupoa..! UEFA Champions League kupigika leo kwa mechi za kibabe
23h ago
READ MORE →
Kapama: Doumbia ndiye aliyeibadilisha Simba jana
Kapama: Doumbia ndiye aliyeibadilisha Simba jana
1d ago
READ MORE →
Simba imetupa funzo - Mgunda
Simba imetupa funzo - Mgunda
1d ago
READ MORE →
Yanga mbioni kumtangaza kocha mpya
Yanga mbioni kumtangaza kocha mpya
1d ago
READ MORE →