Arsenal yatepeta mbele ya Man City fainali kombe la Carabao

Joel JJ By Joel JJ
•
22 Mar 2026
Arsenal yatepeta mbele ya Man City fainali kombe la Carabao

Manchester City imeibuka bingwa wa EFL Cup 2026 Final baada ya kuifunga Arsenal mabao 2-0 katika fainali iliyochezwa leo Jumapili kwenye Uwanja wa Wembley.

Mabao yote mawili yalifungwa na Nico O’Reilly, ambaye alionekana kwa kiwango cha juu, akiwa shujaa wa mechi. Bao la kwanza liliibuka dakika ya 60 baada ya kipa wa Arsenal, Kepa Arrizabalaga, kushindwa kudhibiti mpira wa krosi, huku bao la pili likifungwa dakika ya 64 kwa kichwa kufuatia shambulizi la kujibu la Manchester City. O’Reilly alitangazwa mchezaji bora wa mechi (Man of the Match).

Manchester City, chini ya kocha Pep Guardiola, walitawala kipindi cha pili cha mchezo, wakitumia nafasi zao vizuri na kuonyesha mpangilio bora wa mashambulizi. Kipa wao, James Trafford, alifanya uokoaji muhimu kadhaa na kuzuia Arsenal kurejea kwenye mechi.

Kwa upande wa Arsenal, walijitahidi lakini walikosa umakini katika kumalizia nafasi. Wachezaji kama Declan Rice walishindwa kuleta tofauti, na makosa ya kipa wao yalichangia City kuibuka bingwa.

Ushindi huu unaipa Manchester City taji lao la kwanza la ndani msimu huu, huku wakionesha ubabe na uthabiti mkubwa katika soka la Uingreza. Kwa Arsenal, matokeo haya ni pigo, huku wakiendelea kupigania mataji mengine yaliyosallia Ligi Kuu na UEFA CL.

Bado Arsenal na City zinachuana kuwania taji la ligi kuu ingawa Arsenal ikionekana kuwa na nafasi ya wazi zaidi kumaliza ukame wa taji hilo

ADVERTISE HERE

More Stories

Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
31m ago
READ MORE →
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
1h ago
READ MORE →
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
4h ago
READ MORE →
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
6h ago
READ MORE →
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
7h ago
READ MORE →
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
7h ago
READ MORE →
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
9h ago
READ MORE →
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
9h ago
READ MORE →
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
9h ago
READ MORE →
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
22h ago
READ MORE →