Barcelona yarudi kileleni La Liga baada ya ushindi dhidi ya Levante

Joel JJ By Joel JJ
•
23 Feb 2026
Barcelona yarudi kileleni La Liga baada ya ushindi dhidi ya Levante

Klabu ya FC Barcelona imerejea kileleni mwa msimamo wa La Liga baada ya kuichapa Levante UD mabao 3-0 katika mchezo uliochezwa Jumapili, Februari 22, 2026.

Katika mechi hiyo iliyopigwa uwanja wa Camp Nou, Barcelona ilianza kwa kasi na kupata bao la mapema dakika ya nne kupitia kwa kiungo chipukizi Marc Bernal. Bao hilo liliwapa wenyeji kujiamini na kuendelea kuutawala mchezo kwa umiliki mkubwa wa mpira.

Dakika ya 32, kiungo wa kimataifa wa Uholanzi Frenkie de Jong aliifungia Barcelona bao la pili baada ya shambulizi lililopangwa vizuri. Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa Barcelona kuwa mbele kwa mabao 2-0.

Kipindi cha pili, Levante walijaribu kusawazisha hali ya mchezo lakini safu ya ulinzi ya Barcelona ilisimama imara. Dakika ya 81, Fermín López alifunga bao la tatu na kuthibitisha ushindi huo muhimu kwa wenyeji.

Kwa ushindi huo, Barcelona imefikisha pointi 61 baada ya mechi 25 na kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi, wakiwa pointi moja mbele ya wapinzani wao wakuu, Real Madrid CF. Matokeo hayo yanaongeza presha katika mbio za ubingwa huku msimu ukiingia katika hatua ya mwisho.

Kwa upande wa Levante, matokeo hayo yanawaacha katika hali ngumu kwenye vita ya kujinusuru kushuka daraja, huku wakizidi kuporomoka katika msimamo wa ligi.

ADVERTISE HERE

More Stories

Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
14m ago
READ MORE →
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
2h ago
READ MORE →
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
5h ago
READ MORE →
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
6h ago
READ MORE →
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
6h ago
READ MORE →
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
7h ago
READ MORE →
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
8h ago
READ MORE →
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
8h ago
READ MORE →
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
21h ago
READ MORE →
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE →