Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne, Februari 10 2026

Joel JJ By Joel JJ
β€’
10 Feb 2026
Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne, Februari 10 2026

Cristiano Ronaldo anatarajiwa kusitisha mgomo wake katika klabu ya Al-Nassr na kucheza tena katika klabu hiyo ya Saudi Pro League siku ya Jumamosi. Fowadi huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 41 amekosa mechi mbili kwa sababu hakufurahishwa na jinsi klabu hiyo inavyoendeshwa. (Sky Sports)

Hatma ya mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Marcus Rashford Barcelona inategemea uchaguzi wa rais wa klabu hiyo mwezi ujao. Mkataba wa pauni milioni 26 kwa mshambuliaji huyo wa Manchester United kwa mkopo, 28, ndio kiini cha ombi la Joan Laporta kuchaguliwa tena. (Times - Subscription Required)

Manchester United itamlenga mshambuliaji wa Everton na Senegal Iliman Ndiaye, 25, ikiwa Rashford atahamia Barcelona kwa mkataba wa kudumu. (Caught Offside)

Bournemouth inapanga kumpa mshambuliaji wa Ufaransa Eli Junior Kroupi, 19, kandarasi mpya yenye unono mwingi kwa nia ya kuzuia kutakiwa na baadhi ya vilabu vikubwa barani Ulaya, vikiwemo Chelsea, Liverpool, Real Madrid na Paris St-Germain. (Sun)

'Manchester City wanajiandaa kutoa kitita cha pauni milioni 100 kwa ajili ya kumnunua kiungo wa kati wa Nottingham Forest Muingereza Elliot Anderson, 23. (Teamtalks)

Bayern Munich hawatarajii kumsaini fowadi wa Atletico Madrid na Argentina Julian Alvarez, na hivyo kuongeza matumaini ya Arsenal kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Christian Falk)

AC Milan wana imani kuwa Fulham watatoa chaguo la pauni milioni 21 kumnunua winga wa Nigeria Samuel Chukwueze, 26, ambaye yuko kwa mkopo Cottagers. (Gazzetta - In Italy)

Manchester United wanamtaka kiungo wa kati wa Borussia Monchengladbach Mjerumani Rocco Reitz, 23, ambaye thamani yake ni takriban Β£35m. (Fichajes - In Spanish)

Mchezaji mwengine anayelengwa na Manchester United, Sandro Tonali wa Newcastle United, huenda akawa na bei ya hadi Β£100m. Kiungo huyo wa kati wa Italia mwenye umri wa miaka 25 pia anavutia klabu za Arsenal, Manchester City na Juventus. (Talksport)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
45m ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
2h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
3h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
4h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
5h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
7h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
9h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
10h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
11h ago
READ MORE β†’