Twiga Stars yatupwa nje WAFCON 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
15 Jul 2025
Twiga Stars yatupwa nje WAFCON 2024

Timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania, maarufu kama Twiga Stars, imehitimisha safari yake katika michuano ya WAFCON 2024 baada ya kuondolewa rasmi kufuatia kipigo cha mabao 4-1 dhidi ya Ghana katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi uliochezwa nchini Morocco.

Katika mchezo huo wa mwisho wa kundi C, Twiga Stars ilikuwa na kazi moja t, kupata ushindi ili kujiweka hai kwenye mashindano, lakini matumaini hayo yalizimwa na vijana wa Ghana waliotawala mchezo kwa kiasi kikubwa.

Bao pekee la Twiga lilifungwa na Stumai Abdallah, huku Ghana wakifunga kupitia kwa Pricella Adubea, Alice Kusi, Evelyn Badu, na Chantelle Boye.

Kwa matokeo hayo, Twiga Stars imemaliza hatua ya makundi ikiwa nafasi ya mwisho kwenye kundi C kwa pointi moja tu waliyoipata baada ya kutoka sare dhidi ya Banyana Banyana ya Afrika Kusini.

Afrika Kusini imemaliza kileleni mwa kundi hilo kwa pointi saba, ikifuatiwa na Ghana yenye pointi nne sawa na Mali, lakini Ghana wakinufaika kwa uwiano mzuri wa mabao na hivyo kusonga mbele.

Hii inaashiria safari ngumu kwa Twiga Stars, ambayo licha ya jitihada zao, haikuweza kufanikisha malengo ya kuvuka hatua ya makundi kwenye mashindano haya makubwa ya bara la Afrika.

ADVERTISE HERE

More Stories

Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
39m ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
1h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
2h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
4h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
6h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
7h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
8h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
9h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
10h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
10h ago
READ MORE β†’