Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu Julai 07 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
7 Jul 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu Julai 07 2025

Chelsea wanatarajia kupokea ofa ya zaidi ya pauni milioni 50 kwa ajili ya mshambuliaji wao wa England mwenye umri wa miaka 23, Noni Madueke, ambaye amekubaliana masharti binafsi na Arsenal kuhusu uhamisho. (Telegraph)

Mshambuliaji wa Sporting mwenye umri wa miaka 27 kutoka Sweden, Viktor Gyokeres, yuko tayari kutoa takriban pauni milioni 2 za mshahara wake ili kusaidia uhamisho wake wa pauni milioni 70 kwenda Arsenal. (Record)

Tottenham na West Ham bado wako kwenye mazungumzo kuhusu uhamisho wa kiungo wa Ghana, Mohammed Kudus, baada ya West Ham kukataa ofa ya awali ya pauni milioni 50 kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Sky Sports)

Borussia Dortmund wanataka kuongeza mkataba wa mkopo wa kiungo wa Chelsea, Carney Chukwuemeka, mwenye umri wa miaka 21, huku kipengele cha kumtoa kwa pauni milioni 40 mchezaji huyo kinda wa England kikifanya uhamisho wa kudumu kuwa mgumu. (Talksport)

Mshambuliaji wa Nigeria, Victor Osimhen, yuko tayari kujiunga na Galatasaray, ambako alikuwa kwa mkopo msimu uliopita, lakini klabu hiyo ya Uturuki italazimika kuilipa Napoli pauni milioni 65 ili kumsajili, kwani klabu hiyo ya Italia haiko tayari kumtoa chini ya hapo. (Corriere dello Sport)

Crystal Palace wako karibu kukamilisha usajili wa beki wa kushoto wa Ajax mwenye umri wa miaka 27, Borna Sosa, kwa pauni milioni 2. (Athletic)

Mshambuliaji wa Koln, Damion Downs, anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya Southampton Jumanne. Mmarekani huyo mwenye umri wa miaka 21 atasaini mkataba wa miaka minne na klabu hiyo ya Championship. (Florian Plettenberg)

Roma wanavutiwa na kumsajili kiungo wa Brighton na Denmark mwenye umri wa miaka 24, Matt O'Riley. (La Gazetta Dello Sport) Leeds wanavutiwa na Anton Stach wa Hoffenheim lakini huenda watakabiliwa na ushindani wa kumsajili kiungo huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 26. (Kicker)

Kiungo wa Everton mwenye umri wa miaka 35 kutoka Senegal, Idrissa Gueye, amesaini mkataba mpya utakaodumu hadi 2027. (Fabrizio Romano)

Mkurugenzi wa michezo wa Genoa, Flavio Ricciardella, alikubaliana na mkataba wa kumsajili Jamie Vardy, lakini meneja Patrick Vieira alikataa uhamisho wa mshambuliaji huyo wa zamani wa England mwenye umri wa miaka 38, ambaye aliachwa na Leicester wiki iliyopita. (La Repubblica)

Norwich wamekubali mkataba wa kumsajili beki wa Denmark mwenye umri wa miaka 23, Mathias Kvistgaarden, kutoka Brondby. (Tipsbladet)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
5h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
7h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
7h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
8h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
9h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
9h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
12h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
14h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
15h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
15h ago
READ MORE β†’