Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne June 03 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
3 Jun 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne June 03 2025

Mshambulizi wa Brentford Bryan Mbeumo anataka kujiunga na Manchester United , ambayo sasa iko tayari kuanzisha mazungumzo ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon mwenye umri wa miaka 25. (Subscription requires)

Inter Milan wanatumai kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na Denmark Rasmus Hojlund, 22, kwa mkopo msimu huu. (Gazzetta dello Sport - In Italic)

Manchester United pia inasubiri uamuzi kutoka kwa kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes kuhusu kama anataka kusalia katika klabu hiyo au kuondoka, huku klabu ya Saudi Arabia Al-Hilal ikimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. (Sky Sports)

Mshambulizi wa Crystal Palace Mfaransa Jean-Philippe Mateta, 27, pia yuko kwenye orodha ya washambuliaji wa Manchester United , lakini huenda wakakabiliwa na ushindani kutoka kwa Juventus na AC Milan . (TeamTalk)

Myles Lewis-Skelly, 18, anatarajiwa kusaini kandarasi mpya na Arsenal msimu huu wa kiangazi, huku The Gunners wakiwa na nia ya kuzuia tetesi za kutaka kumnunua beki huyo wa Uingereza kutoka Real Madrid . (Mirror)

Liverpool wamekubali mkataba na kiungo wa kati wa Ujerumani Florian Wirtz hadi 2030, lakini bado hawajakubali ada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, huku Bayer Leverkusen wakikataa ofa ya euro 130m (Β£110m) kutoka kwa Reds huku wakishikilia euro 150m (Β£127m). (Bild - in German)

Barcelona wameanza mazungumzo ya awali na winga wa Liverpool Luis Diaz, 28, wakimtaka Saudi Arabia kumnunua mchezaji huyo wa Colombia. (Florian Plettenberg)

Chelsea wanafikiria kumnunua mlinzi wa kati wa Everton na England Jarrad Branthwaite, 22, wakati Tottenham wanaweza kushindana na The Blues kuwania saini yake msimu huu wa kiangazi. (TeamTalk)

Kiungo wa kati wa Uingereza Jobe Bellingham amechagua kujiunga na klabu ya zamani ya kaka yake Jude Borussia Dortmund badala ya Eintracht Frankfurt na RB Leipzig na klabu hiyo ya Ujerumani itaanza mazungumzo na Sunderland kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19. (Bild - in Germany)

Manchester City wanakaribia kufikia makubaliano ya kumnunua kiungo wa kati wa AC Milan na Uholanzi Tijjani Reijnders, 26, kwa ajili ya Kombe la Dunia la Klabu la Fifa litakaloanza Juni 14 nchini Marekani. (Football Italia)

Chelsea pia wanafikiria kumnunua winga wa Borussia Dortmund Muingereza Jamie Gittens, 20, ambaye anaweza kugharimu takriban Β£50m. (Guardian)

Everton, Manchester United na West Ham wanaweza kumnunua mshambuliaji wa Serbia Aleksandar Mitrovic, huku Al-Hilal wakiwa tayari kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. (Sport)

Kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal na England Jack Wilshere, 33, ndiye mtangulizi wa kuwa meneja wa League One Plymouth Argyle . (Sun)

Brighton wanafuatilia mwenendo wa kiungo wa kati wa Sheffield United Ollie Arblaster, 21, anapoendelea kupata nafuu kutokana na jeraha . ( TeamTalk )

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

TFF kusimamia uchaguzi wa Simba, ratiba kuboreshwa
TFF kusimamia uchaguzi wa Simba, ratiba kuboreshwa
8m ago
READ MORE β†’
Matola: Namungo ni timu imara, tunataka kutetea rekodi yetu
Matola: Namungo ni timu imara, tunataka kutetea rekodi yetu
3h ago
READ MORE β†’
Tunakwenda kucheza na timu mzito na ngumu: Juma Mgunda
Tunakwenda kucheza na timu mzito na ngumu: Juma Mgunda
3h ago
READ MORE β†’
Jack Grealish aingia matatani Everton baada ya kuripotiwa kula bata siku mbili mfululizo
Jack Grealish aingia matatani Everton baada ya kuripotiwa kula bata siku mbili mfululizo
4h ago
READ MORE β†’
NBC Premier League: Mechi mbili za kibabe kupigwa leo.
NBC Premier League: Mechi mbili za kibabe kupigwa leo.
5h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya mechi kubwa inaendelea: Liverpool vs Arsenal na Napoli vs Juventus
Wikiendi ya mechi kubwa inaendelea: Liverpool vs Arsenal na Napoli vs Juventus
6h ago
READ MORE β†’
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
18h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
20h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
21h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
21h ago
READ MORE β†’