Singida Black Stars yaipania Simba

Joel JJ By Joel JJ
β€’
26 May 2025
Singida Black Stars yaipania Simba

Kocha wa Singida Black Stars raia wa Kenya, David Ouma amesema mechi ya kirafiki dhidi ya Yanga imewapa morali wachezaji wakati huu wakijiandaa kucheza na Simba katika mechi mbili za Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho (FA).

Katika mechi hiyo iliyopigwa Alhamisi iliyopita kwenye Uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge, Dar es Salaam, Singida ilishinda kwa mabao 3-2 yaliyofungwa na Elvis Rupia, Jonathan Sowah na Arthur Bada, huku yale ya Yanga yakifungwa na Prince Dube na Denis Nkane.

Ouma amesema kwa sasa wachezaji wote wako katika hali nzuri na utimamu wa kimwili, na wapo tayari kucheza na Simba katika mechi hizo muhimu zijazo, licha ya kukiri ugumu uliopo kutokana na ubora wa wapinzani wao.

"Tunakwenda kucheza mechi mbili mfululizo na Simba ambazo kwetu tunazichukua kwa umuhimu mkubwa sana. Malengo yetu makubwa yalikuwa ni kupata tiketi ya CAF ambayo tayari tumefanikiwa sasa kilichobaki ni kuendeleza heshima yetu," alisema.

Kocha huyo alisema licha ya ugumu wa mechi hiyo, lakini watapambana kuonyesha ushindani mkubwa wakianzia na ya Ligi Kuu Mei 28 kwenye Uwanja wa KMC Complex kisha na ile ya nusu fainali ya Kombe la FA itakayopigwa Mei 31.

Timu hiyo imepata tiketi ya kushiriki michuano ya CAF msimu ujao baada ya Yanga kuifunga JKT Tanzania kwa mabao 2-0 katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA, hivyo kujihakikishia kumaliza nafasi ya tatu au ya nne msimu huu.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

More Stories

Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
46m ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
3h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
5h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
6h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
6h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
8h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
9h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
9h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
21h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’