Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu May 19 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 May 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu May 19 2025

Manchester United imewasilisha ofa ya euro milioni 65 kumsajili mshambuliaji wa Brentford na Cameroon Bryan Mbeumo, 25, ambaye amesalia na mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa sasa. (Fichajes - kwa Kihispania)

Mshambuliji wa Al-Nassr Cristiano Ronaldo, 40, amepokea ofa kutoka kwa klabu ya Brazil ambayo haijafichuliwa, ambayo ingemruhusu nyota huyo wa Ureno kucheza Kombe la Dunia la Klabu ya Fifa litakaloanza Juni. (Marca - kwa Kihispania)

Aston Villa inavutiwa na mshambuliaji wa Barcelona Ferran Torres, 25, na ipo tayari kutoa takriban euro milioni 50 (Β£42m) kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

Winga wa Lyon mwenye umri wa miaka 21 Mfaransa Rayan Cherki, anayewaniwa na Manchester United na Liverpool, amethibitisha kuwa ataondoka katika klabu hiyo ya Ufaransa msimu huu wa kiangazi. (Goal)

Manchester United pia inataka kumsajili kiungo wa Sporting na Ureno Pedro Goncalves, 26, msimu huu wa kiangazi. (Team talk)

Atletico Madrid ni miongoni mwa klabu kadhaa zinazomtaka kiungo wa kati wa Aston Villa Muargentina Enzo Barrenechea, 23, ambaye anakipiga Valencia kwa mkopo. (Birmingham Mail)

Bayern Munich ina matumaini ya kusalia na winga wa zamani wa Manchester City Leroy Sane huku kandarasi ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 29 akitarajiwa kumalizika mwezi ujao. (Bild - kwa Kijerumani)

Nottingham Forest ina nia kuwapa mkataba mpya wachezaji wawili wa Uingereza, kiungo Morgan Gibbs-White, 25, na winga Callum Hudson-Odoi, 24, haraka iwezekanavyo. (Football Insider)

Napoli inamsaka kiungo mshambuliaji mpya kwa ajili ya msimu ujao na inapanga kumsajili mshambuliaji wa Lille wa Canada Jonathan David, 25, au mshambuliaji wa Liverpool wa Uruguay Darwin Nunez, 25. (Calciomercato - kwa Kiitaliano).

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
13m ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
2h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
4h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
5h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
6h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
7h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
8h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
8h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
21h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’