Simba kuisaka fainali CAF CC leo

Joel JJ By Joel JJ
β€’
27 Apr 2025
Simba kuisaka fainali CAF CC leo

Leo hii katika uwanja wa Moses Mabhida mjini Durban, mechi ya kukata na shoka itapigwa wakati Stellenbosch FC wakimenyana na Simba SC katika mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF.

Simba wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na faida ya ushindi wa bao 1-0 walioupata katika mchezo wa kwanza uliofanyika wiki iliyopita kwenye Uwanja wa New Amaan huko Zanzibar.

Kwa ushindi au sare yoyote, Simba watafuzu kwa mara ya pili katika historia yao kucheza fainali ya michuano ya CAF.

Katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya mechi, Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids, alisema kuwa ana imani kubwa na timu yake na ana uhakika wa kupata matokeo mazuri katika mchezo wa leo

Davids alisisitiza kuwa ni muhimu kwa Simba kufunga bao la ugenini mapema ili kuimaliza mechi hiyo na kupunguza presha.

Kwa upande wa Stellenbosch, huu ni mchezo wa kihistoria kwao, na watahitaji kucheza kwa bidii mbele ya mashabiki wao kujaribu kugeuza matokeo

Hata hivyo, haitakuwa rahisi kwao kwani imeonekana katika mechi zilizopita Simba imeimarika sana katika mechi za ugenini viungo washambuliaji Elie Mpanzu na Kibu Denis wakiwa silaha muhimu kwa Simba katika mechi hizo

Ni wazi leo Stellenbosch watalazimika kushambulia kutafuta mabao, kufunguka kwao kutatoa mwanya kwa Simba kupitia kina Mpanzu, Kibu, Ahoua na wengine kuwaadhibu

Simba inatarajiwa kupata sapoti kubwa ya mashabiki pengine kuliko wenyeji wao kwani mji wa Durban kuna Watanzania wengi ambao wamehamashika kwenda kuishangilia Simba katika mchezo huo

Stellenbosch wanatokea mji wa Cape Town hivyo nao ni kama wageni tu hapo Durban na zaidi sio timu maarufu Afrika Kusini hivyo hawana mashabiki wengi

Ni saa 9 Alasiri (saa 10 Tanzania) ndio muda ambao mtanange huo utapigwa

ADVERTISE HERE

More Stories

Matola: Namungo ni timu imara, tunataka kutetea rekodi yetu
Matola: Namungo ni timu imara, tunataka kutetea rekodi yetu
2h ago
READ MORE β†’
Tunakwenda kucheza na timu mzito na ngumu: Juma Mgunda
Tunakwenda kucheza na timu mzito na ngumu: Juma Mgunda
2h ago
READ MORE β†’
Jack Grealish aingia matatani Everton baada ya kuripotiwa kula bata siku mbili mfululizo
Jack Grealish aingia matatani Everton baada ya kuripotiwa kula bata siku mbili mfululizo
2h ago
READ MORE β†’
NBC Premier League: Mechi mbili za kibabe kupigwa leo.
NBC Premier League: Mechi mbili za kibabe kupigwa leo.
3h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya mechi kubwa inaendelea: Liverpool vs Arsenal na Napoli vs Juventus
Wikiendi ya mechi kubwa inaendelea: Liverpool vs Arsenal na Napoli vs Juventus
5h ago
READ MORE β†’
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
17h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
19h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
19h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
20h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
21h ago
READ MORE β†’