Arsenal yaisambaratisha Manchester City Emirates

Joel JJ By Joel JJ
β€’
3 Feb 2025
Arsenal yaisambaratisha Manchester City Emirates

Arsenal imefufua matumaini katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kuwachapa wapinzani wao Manchester City mabao 5-1 Jumapili usiku

Ni kipigo cha aibu ambacho kinawafanya The Gunners kulipiza kisasi dhidi ya mabingwa hao

Mvutano kati ya timu hizo ulikuwa mkubwa baada ya sare ya 2-2 Septemba lakini hatimaye Arsenal wamepata ushindi dhidi ya vijana wa Pep Guardiola, ambao walikuwa wamebeba ubingwa katika misimu miwili iliyopita

Mabao kutoka kwa vijana Myles Lewis-Skelly na Ethan Nwaneri yalihakikisha ushindi wa kishindo kwa kikosi cha Mikel Arteta, baada ya Martin Odegaard kuwafungia Arsenal mapema ndani ya dakika mbili

Erling Haaland alisawazisha katika kipindi cha pili lakini Arsenal walirudisha faida yao ndani ya sekunde 38 baada ya kuanza tena bao la Thomas Partey likimpita John Stones

Lewis-Skelly aliongeza dakika tatu baadaye likiwa bao lake la kwanza la Arsenal, kabla ya kuonekana kumdhihaki Haaland kwa kunakili aina yake ya ushangiliaji

Kai Havertz alifunga bao la nne kabla ya Nwaneri kuingia akitokea benchi kukamilisha kipigo cha aibu kwa mabingwa hao na kupunguza uongozi wa Liverpool kileleni mwa jedwali

Arsenal imefikisha alama 50 katika nafasi ya pili Liverpool wakiwa kileleni na alama 56

ADVERTISE HERE

More Stories

De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
2h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
4h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
5h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
6h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
6h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
9h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
11h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
12h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
12h ago
READ MORE β†’