Singida Black Stars yamtangaza Miloud

Joel JJ By Joel JJ
β€’
31 Dec 2024
Singida Black Stars yamtangaza Miloud

Klabu ya Singida Black Stars imetangaza kumuajiri kocha Hamdi Miloud mwenye Uraia wa nchi mbili za Ufaransa na Algeria

Miloud anatua kurithi mikoba ya Patrick Aussems ambaye kibarua chake kilisitishwa na timu hiyo baada ya mfululizo wa matokeo mabaya

Taarifa iliyotolewa na Singida BS jana imethibitisha maamuzi hayo'

"Tunapenda kumtambulisha Kocha Mkuu mpya wa Kikosi chetu, Kocha Hamdi Miloud mwenye Uraia wa nchi mbili za Ufaransa na Algeria"

"Kocha Hamdi atasaidiwa na Makocha Wasaidizi wawili; Kocha Nassim Anisse na Kocha David Ouma, katika kukinoa kikosi chetu kuanzia timu itakaporejea kutoka mapumzikoni Januari, 2025"

"Aliyekuwa Kaimu Kocha Mkuu, Ramadhani Nsanzurwimo, amerejea kwenye majukumu yake kama Mkurugenzi wa Ufundi. Kocha Hamdi ana rekodi nzuri ya kufika Hatua ya Fainali katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League - Finals), Robo Fainali mara mbili Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL Quarter Finals) na Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC Quarter Finals)"

"Vilevile, Kocha Hamdi ana uzoefu mkubwa na Soka la Afrika kwa kuzinoa klabu mbalimbali kwa mafanikio makubwa barani Afrika zikiwemo USM Alger na JS Kabylie za Algeria, Al- Salmiya ya Kuwait, TP Mazembe ya Congo, Athletico Marseille na ES Vitrolles za Ufaransa na Al- Ettifaq FC ya Saudia Arabia"

ADVERTISE HERE

More Stories

Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
2h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
4h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
5h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
5h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
7h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
8h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
8h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
20h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
1d ago
READ MORE β†’