Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa Novemba 29 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
29 Nov 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa Novemba 29 2024

Winga wa Liverpool na Misri Mohamed Salah, 32, ndiye 'ndoto' ya usajili wa Saudi Pro League msimu ujao. (Mail - Subscription Required)

Manchester United wanapanga uhamisho wa pauni milioni 50 ili kuwashinda Chelsea kwa ajili ya kumnunua beki wa kati wa Benfica na Ureno Tomas Araujo, 22, mwezi Januari. (Sun)

Beki wa Crystal Palace, 24, Muingereza, Marc Guehi, anatamani kujiunga tena na Chelsea, wakati Newcastle pia bado wanavutiwa na beki huyo wa kati. (TeamTalks)

Hatua ya Arsenal ya kutaka mshambuliaji mpya imepata pigo kwa Viktor Gyokeres, 26, anayetaka kumfuata meneja wa zamani wa Sporting Lisbon Ruben Amorim kwenda Manchester United. (Football.London)

The Gunners wana takriban washambuliaji sita kwenye orodha ya wachezaji inaowalenga , akiwemo mshambuliaji wa Newcastle United na Uswidi Alexander Isak, 25. (Caught Offside)

Manchester City na Manchester United wamepewa fursa ya kumnunua kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz, 26, na kiungo wa kati wa Italia na Juventus Fagioli, 23, . (Gazzetta dello Sport - In Itali)

Meneja wa Chelsea Enzo Maresca amekanusha kuwa Christopher Nkunku anauzwa, licha ya fowadi huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 27 kuwa na muda mfupi wa kucheza. (Times - Subnscription Required)

Fowadi wa Paraguay Miguel Almiron, 30, ataruhusiwa kuondoka Newcastle mwezi Januari. (Telegraph - Subscription Required)

Manchester City pia inamfuatilia kiungo wa kati wa Borussia Monchengladbach Mjerumani Rocco Reitz mwenye umri wa miaka 22 juu ya uwezekano wa kuhama mwezi Januari. (GiveMeSport), nje Napoli wameiuliza Arsenal kuhusu upatikanaji wa beki wa Poland Jakub Kiwior, 24, kwa mkopo mwezi Januari. (Gianluca di Marzio, via Metro)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
14m ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
2h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
5h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
6h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
6h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
7h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
8h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
8h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
21h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’