Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi Oktoba 17 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
17 Oct 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi Oktoba 17 2024

Real Madrid wameufanya usajili wa mlinzi wa Liverpool na Uingereza Trent Alexander-Arnold, 26, kuwa kipaumbele. (Athletic – Subscription needed) Liverpool na Manchester City wanavutiwa na Nicolo Barella wa Inter Milan, 27, lakini kiungo huyo wa kati wa Italia yuko kwenye rada za Real Madrid na Atletico Madrid. (Fichajes – In Spanish)

Arsenal wanafuatilia maendeleo ya mshambuliaji wa Red Bull Salzburg na Slovenia Benjamin Sesko, 21, huku wakianza kujipanga kwa ajili ya usajili wa dirisha lijalo. (Football London)

Crystal Palace haiko tayari kukaribisha ofa zozote kwa mshambuliaji wa Senegal Ismaila Sarr, 26, mwezi Januari. (Football Insider)

Manchester United wamemuongeza mkufunzi wa Uturuki na mshambuliaji wa zamani wa Italia Vincenzo Montella, 50, kwenye orodha yao ya watu wanaotarajiwa kuchukua nafasi ya mkufunzi wa Uholanzi Erik ten Hag, 54, Old Trafford. (Ajansspor – in Turkish)

Ten Hag atalazimika kuboresha matokeo na kiwango cha mchezo Manchester United ikiwa anataka kusalia katika timu hiyo baada ya mapumziko yajayo ya kimataifa. (Mirror), nje

Manchester United wanapanga wachezaji wa kiungo cha kati watakaochukua nafasi ya kiungo wa kimataifa wa Denmark Christian Eriksen, 32, pamoja na mchezaji wa kimataifa wa Brazil Casemiro, 32. (Football Insider)

United pia wako tayari kumsajili kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong, 27, ikiwa ataondoka Barcelona msimu ujao. (Fichajes – In Spanish)

Real Madrid wanafikiria kumnunua mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Josh Acheampong Januari 18, huku Liverpool, Newcastle na Tottenham pia wakimtaka beki huyo wa kulia wa Chelsea. (Independence)

Crystal Palace wanamtafuta David Moyes, 61, kuchukua nafasi ya meneja Oliver Glasner, 50, baada ya kuanza vibaya msimu wa Ligi Kuu ya Uingereza. (Caughtoffside)

Uteuzi wa Thomas Tuchel kama meneja wa Uingereza umeongeza matumaini ya Newcastle ya kumsajili mlinzi wa Uingereza na Crystal Palace Marc Guehi, 24, huku Eddie Howe sasa akiwa na uwezekano mkubwa wa kusalia St James' Park. (Givemesport)

Liverpool wako kwenye mazungumzo na Sevilla kuhusu kumnunua mlinzi wa Ufaransa Loic Bade, 24. (Todo Fichajes – In Spanish)

Kiungo wa kati wa Newcastle United Isaac Hayden, 29, amekubali kuiwakilisha Jamaica katika ngazi ya kimataifa, baada ya hapo awali kuichezea Uingereza katika kila kundi la umri kutoka chini ya miaka 16 hadi chini ya miaka 21. (TeamTalks)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
1h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
1h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
2h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
3h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
4h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
6h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
8h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
9h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
10h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
11h ago
READ MORE β†’