Adebayor tayari kuitumikia Singida BS

Joel JJ By Joel JJ
β€’
23 Sep 2024
Adebayor tayari kuitumikia Singida BS

Kocha Mkuu wa Singida Black Stars, Patrick Aussems amesema kwa sasa nyota mpya wa kikosi hicho, Victorien Adebayor yupo tayari kuanza kuitumikia timu hiyo baada ya awali kumpa programu maalumu kwa ajili ya kujiweka fiti

Adebayor aliyejiunga na timu hiyo msimu huu akitokea AS GNN ya kwao Niger aliyojiunga nayo Januari mwaka huu kwa mkopo akitoka AmaZulu FC ya Afrika Kusini, hajacheza mchezo wowote ndani ya kikosi hicho baada ya kupewa programu maalumu

"Adebayor alihitaji muda zaidi kwa sababu alichelewa kujiunga na wenzake kutokana na changamoto za kifamilia, ilibidi abaki Singida kwanza na tunashukuru maendeleo yake kwa sasa ni mazuri na yupo tayari kucheza kikosini," alisema Aussems

Aussems aliongeza, Adebayor atajiunga na mazoezi ya moja kwa moja na mwenzake waliowasili jana mjini Singida na atakuwa sehemu ya kikosi kitakachohusika katika mchezo ujao wa timu hiyo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania Septemba 29

Singida imerejea mjini Singida ikitokea Mwanza ilipoibuka na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Pamba Jiji na kuifanya timu hiyo kuendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kufikisha jumla ya pointi 12 katika michezo minne

Uwepo wa nyota huyo unaongeza machaguo mengi kwa Aussems kutokana na Adebayor kucheza katika wingi zote mbili kwa ufasaha kwa maana ya kulia na kushoto huku akicheza pia kama mshambuliaji wa kati, eneo waliopo mastaa, Elvis Rupia na Joseph Guede

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

More Stories

Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
47m ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
3h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
5h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
6h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
6h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
8h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
9h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
9h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
21h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’