Makocha 21 wajitosa kumrithi Dabo Azam Fc

Joel JJ By Joel JJ
β€’
4 Sep 2024
Makocha 21 wajitosa kumrithi Dabo Azam Fc

Zikiwa zimepita saa 24 tangu klabu ya Azam Fc itangaze kumfuta kazi kocha Yusuph Dabo na benchi lake la ufundi, takribani makocha 21 wametuma 'CV' Azam Fc kwa ajili ya kumrithi kocha huyo raia wa Senegal

Afisa Habari wa Azam Fc Hashim Ibwe amesema wamepokea maombi kutoka kwa makocha 21 ambapo tayari mchujo wa kwanza umefanyika na kubakisha makocha wanne

Ibwe amesema ndani ya siku mbili watatamtangaza mrithi wa Dabo ambaye atakuwa takribani wiki moja ya kukiandaa kikosi chake kabla ya ratiba ya ligi kuu kuendelea baada ya mapumziko ya kalenda ya FIFA

"Tumepokea maombi kutoka kwa makocha 21, mchujo umefanyika na kubakisha majina ya makocha wanne ambao watapitia katika mchujo mwingine ili kumpata mrithi wa kocha aliyeondoka"

"Kama kila kitu kitakwenda sawa, tutamtangaza kocha mpya ndani ya muda wa siku mbili zijazo"

"Tunataka kocha mpya ajiunge nasi wakati huu ambao ligi imesimama ili apate angalau siku chache za kufanya mazoezi na timu," alisema Ibwe

Jana Azam Fc ilitangaza kumfuta kazi Dabo baada mwanzo mbaya wa msimu

Azam Fc ilichapwa mabao 4-1 na Yanga katika mchezo wa fainali ya Ngao ya Jamii kabla ya kukutana na kipigo cha mabao 2-1 katika mechi mbili za hatua ya awali ya ligi ya mabingwa barani Afrika na matajiri hao kutoka Chamazi kutupwa nje ya michuano mapema

Azam Fc ikaanza ligi kwa kuchechemea ikilazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya JKT Tanzania

Miongoni mwa makocha wanaotajwa kuhitajika na Azam Fc ni Florente Ibenge anayeinoa klabu ya Al Hilal ya Sudan

Hivi karibuni Ibenge alikuwa nchini na Al Hilal ambapo walicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Simba

ADVERTISE HERE

More Stories

Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
1h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
3h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
4h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
5h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
6h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
7h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
7h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
20h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
1d ago
READ MORE β†’