Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne Juni 25 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
25 Jun 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne Juni 25 2024

Manchester United wanatazamia kukidhi kipengele cha kuachiliwa kwa Joshua Zirkzee huku wakipanga kumuuza Mason Greenwood ili kufadhili mpango huo, nao Everton wakitakiwa kuwasilisha ombi jingine kwa Jarrad Branthwaite

Manchester United wanatarajiwa kufikia kipengee cha uhamisho cha euro 40m (£33.9m) kwa mshambuliaji wa Bologna Joshua Zirkzee, 23, na pia wamefanya mazungumzo na Lille kuhusu mkataba wa kumnunua beki wa Ufaransa wa U21 mwenye umri wa miaka 18 Leny Yoro. (Sky Sports)

United wanatumai kufadhili usajili wa Zirkzee kwa kumuuza mshambuliaji wa Uingereza Mason Greenwood, 22. (I Sport)

Everton wanatarajia Manchester United itawasilisha ofa nyingine kwa beki wa Uingereza Jarrad Branthwaite, 21. (Liverpool Echo)

Everton wanakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Senegal Iliman Ndiaye, 24, kutoka Marseille. (Footmercato – In French)

Manchester United wanatarajia kukubaliana kandarasi mpya na meneja Erik ten Hag kabla ya kuanza kwa ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya nchini Marekani mwezi ujao. (ESPN)

Mshambulizi wa zamani wa Manchester United Ruud van Nistelrooy, 47, amefanya mazungumzo chanya kuhusu kurejea katika klabu hiyo kama sehemu ya wakufunzi wa Ten Hag. (Talksport)

Mshambuliaji wa Uhispania Joselu, 34, anakaribia kuondoka Real Madrid baada ya kupokea ofa kutoka kwa klabu ya Qatar Al Gharafa. (Athletic – Subscription Required)

Chelsea wameanza mazungumzo na Barcelona kuhusu mkataba wa kumnunua mshambuliaji wa Uhispania Marc Guiu, 18. (ESPN)

The Blues wanaongoza Bayern Munich katika mbio za kumsajili Guiu. (Fabrizio Romano) Borussia Dortmund wanavutiwa na kiungo wa kati wa Leeds United wa U21 Archie Gray, 18. (Bild – In Germany)

Tottenham wameanza mazungumzo na wawakilishi wa mshambuliaji wa Lille wa Canada Jonathan David, 24, ambaye pia anahusishwa na kuhamia Chelsea. (Football Insider)

Mchezaji wa Ghana Mohammed Kudus, 23, amekuwa akihusishwa na kutaka kuondoka West Ham lakini klabu hiyo bado haijapokea ofa ya kiungo huyo mshambuliaji. (Sky Germany)

Napoli itazingatia ofa ya kiwango cha euro 100m (£85m) kwa mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 25, na mshambuliaji wa Chelsea wa Ubelgiji Romelu Lukaku anayetarajiwa kuchukua mahala pake. (Calciomercato – In Italy)

Aston Villa wameungana na Chelsea katika kinyang'anyiro cha kumnunua fowadi wa Hoffenheim Mjerumani Maximilian Beier, 21. (Sky Sport Germany)

Ligi kuu ya Uingereza imezionya klabu kuwa kuuza wachezaji kwa kufuata sheria za kifedha kunaweza kukiuka kanuni za kutenda kwa nia njema. (Times - Subscription Required)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
13m ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
2h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
4h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
5h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
6h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
7h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
8h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
8h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
21h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’